The House of Favourite Newspapers

Kocha Simba azungumza na timu tatu Sauz

0

KERRAliyekuwa kocha wa Simba, Muingereza, Dylan Kerr.

Hans Mloli,
Dar es Salaam
IMEBAINIKA kuwa aliyekuwa kocha wa Simba, Muingereza, Dylan Kerr yupo nchini Afrika Kusini ‘Sauz’ anatafuta timu ya kuinoa.
Taarifa hii ipo tofauti na wanayoijua viongozi wa Simba iliyovuma hivi karibuni kuwa kocha huyo amekwenda kisiwani Pemba akisubiri tiketi yake ya kurejea kwao Uingereza kuendelea na maisha yake mengine.
Kerr ambaye alifungashiwa virago mapema mara baada ya timu yake kutolewa kwenye Kombe la Mapinduzi, yupo nchini humo sasa kwa takriban wiki moja tangu aondoke Tanzania, Januari 20, mwaka huu.
Imeelezwa kwamba, tayari kuna timu tatu kocha huyo anazungumza nazo zinazoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini, ingawa chanzo cha taarifa hii hakikuwa tayari kufafanua zaidi kuhusiana na timu hizo.
Hata hivyo, Simba iliwajibika kama walivyokubaliana kumtumia tiketi Kerr ya kurejea kwao juzi Jumatatu usiku na ikamfikia ingawa imefafanuliwa kuwa tayari amebadili siku ya kuondoka ambapo baada ya kuondoka leo sasa ataondoka siku nyingine ili apate muda zaidi wa kumalizia dili zake.
“Kerr bado hajaenda kwao Uingereza, wengi wanajua yupo Pemba na hata viongozi wa Simba walimtumia tiketi jana (juzi) usiku lakini inavyoonekana Kerr amebadili siku ya kuondoka kwa ajili ya kukamilisha dili zake, kuna timu tatu kule anazungumza nazo,” kilisema chanzo. Championi Jumatano, lilimtafuta kocha huyo ambaye kweli alikiri bado yupo Afrika kwenye mazungumzo na baadhi ya timu ingawa aligoma kuweka wazi yupo nchi gani.
“Bado sijarudi Uingereza, nipo Afrika kuna vitu namalizia kabla ya kurudi Uingereza. Kurejea nyumbani itategemea muda gani nitamalizana na timu ninazozungumza nazo, nikimalizana nao nitakujulisha. Simba walinitumia tiketi yangu jana na nilitakiwa kuondoka jana, lakini haikuwa hivyo,” alisema Kerr ambaye alipotea hewani ghafla baada ya maelezo hayo.
Kerr ameondoka Simba kwa kile kilichoelezwa kuwa uongozi kutoridhishwa na matokeo ya timu hiyo aliyoiongoza kwenye mechi 13 za ligi na kuiacha kwenye nafasi ya tatu ikiwa na pointi 27, tofauti ya pointi sita nyuma ya vinara Yanga na Azam.

Leave A Reply