The House of Favourite Newspapers

Nyota Simba wamfuata daktari wa Cannavaro

0

kiongera1Straika wa Simba, Paul Kiongera.

Said Ally na Omary Mdose
NYOTA wawili wa kikosi cha Simba, straika, Paul Kiongera na beki Mohammed Fakhi, jana Jumanne walipelekwa kwa daktari, Gilbert Kidaye kwa ajili ya kutibiwa majeraha yao.

Daktari huyo wa Hospitali ya Muhimbili, ndiye aliyemtibu beki wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ pamoja na Ibrahim Ajib wa Simba.
Fakhi na Kiongera kwa pamoja wanasumbuliwa na maumivu ya misuli ya paja na wanatarajia kuwa nje ya uwanja kwa wiki moja.
Mratibu wa Simba, Abass Ally, ameliambia Championi Jumatano kuwa, jana baada ya kutoka mazoezi ya asubuhi ambayo nyota hao hawakuwepo, walitarajia kuwapeleka kwa daktari huyo ili kuwaangalia zaidi majeraha yao kabla ya kuanza matibabu.
“Fakhi na Kiongera tumewapeleka kwa daktari Gilbert kuangalia majeraha yao kabla hawajaanza kutibiwa ndiyo maana hawakuwepo mazoezini.
“Lakini pia Tshabalala (Mohammed Hussein ambaye anaumwa goti), yeye tunatarajia kuwa naye kesho (leo) Jumatano katika mazoezi baada ya kumkosa kwa wiki moja,” alisema Ally.

Leave A Reply