The House of Favourite Newspapers

Kocha Simba: Nilijua Nitawafunga Yanga

0

KOCHA Mkuu wa Simba Queens, Sebastian Nkoma, amefunguka kuwa kwa upande wake alikuwa anatambua ni lazima atawafunga wapinzani wake, Yanga Princess katika mchezo wa Ligi Kuu Wanawake lakini hakujua atawafunga kwa idadi gani ya mabao.

 

Katika mchezo huo uliopigwa juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar, Simba Queens iliibuka na ushindi wa mabao 4-1. Simba imeendeleza rekodi yake ya kuifunga Yanga kwenye ligi hiyo kuanzia msimu wa 2018-19.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Nkoma alisema kuwa: “Binafsi nawaheshimu wapinzani wangu kwa sababu kwa misimu miwili nimekuwa nawania nao ubingwa maana wao ni timu kubwa ambayo imekuwa na ushindani mzuri katika hii ligi.

 

“Lakini suala la kuwa leo (juzi) Simba itashinda hilo nilikuwa nalijua wazi japokuwa sikuwa najua kwamba tutashinda kwa idadi kubwa ya mabao ambayo tumeweza kushinda mbele yao.”

IBRAHIM MUSSA, DAR ES SALAAM

Leave A Reply