The House of Favourite Newspapers

Kocha Yanga Akutana na Rungu Jingine Sauz

0

SHIRIKISHO  la Soka la  Afrika Kusini (SAFA) limemfutia jumla vibali vya kazi Luc Eymael aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga kufanya kazi ndani ya nchi hiyo. Imeeleza taarifa kupitia tovuti ya SAFA.

 

Aidha, SAFA imeliomba Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) kumuadhibu zaidi kocha huyo.

 

Eymael, Julai 26 baada ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Lipuli, alisambaza taarifa ambazo zilikuwa zinaonyesha ubaguzi wa rangi na kusema Watanzania hawajui soka.

 

Tayari Yanga imeshamfuta kazi Eymael  kutokana na kitendo hicho na kuomba radhi kwa mashabiki, Serikali na Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF).

 

Kocha huyo pia aliomba msamaha kwa kueleza kuwa alifanya hivyo kutokana na hasira alizokuwa nazo kwa kupitia kipindi kigumu ndani ya Yanga.

 

 

Leave A Reply