The House of Favourite Newspapers

Kocha wa Yanga Miguel Gamondi Afichua Siri Ya 5-1 dhidi ya Simba

0

MARA baada ya kupata ushindi wa mabao 5-1, Kocha Mkuu wa Yanga, Muargentina, Miguel Gamondi, ameibuka na kutaja siri tatu ya ushindi huo kwa timu yake.

Timu hizo zilivaana juzi Jumapili katika mchezo wa Kariakoo Dabi uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam ukiwa ni wa Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na Spoti Xtra, Gamondi alianza kwa kuwapongeza wachezaji wake kwa kucheza kwa kujituma na kutimiza majukumu aliyowapa kabla na wakati mchezo.

Gamondi alitaja siri tatu ambazo ziliwapa ushindi huo, moja ni nidhamu ya uchezaji kwa wachezaji wake wanapokuwa na mpira na wanapoupoteza katika kukaba na kusababisha mpinzani kushindwa kumiliki kwa muda mrefu.

Aliitaja ya pili, vipaji walivyonavyo wachezaji ambavyo vimeamua matokeo hayo wakiongozwa na Pacome Zouzoua, Maxi Nzengeli na Stephane Aziz Ki.

Alimalizia ya tatu ni morali ya kila mchezaji ya kutaka kupata ushindi katika kila mchezo, ambayo anaamini wakiendelea nayo itafikia malengo yao ya msimu huu huku akiwataka wachezaji wake kutobweteka baada ya ushindi.

“Ninawapongeza wachezaji wangu kwa kucheza kwa kufuata maelekezo yangu ambayo nimekuwa nikiwapa katika uwanja wa mazoezi, ninafurahia kuona hilo.

“Baada ya ushindi huu, hatutakiwi kubweteka, bado tuna michezo mingi migumu ya ligi ambayo tunatakiwa kupata ushindi.

“Nimewasisitizia hilo wachezaji wangu, hatutakiwi kuwa na furaha kubwa, kwani mbele tuna kibarua kigumu cha michezo ya ligi na kimataifa,” alisema Gamondi.

AHMED ALLY – ”MWANA SIMBA FANYA UNACHOWEZA UPATE USINGIZI, KUHUSU TIMU YETU TUTAJADILI KESHO”…

Leave A Reply