The House of Favourite Newspapers

Kocha Yanga Ashusha Mshambuliaji

KOCHA Mkuu wa Yanga Mkongomani, Mwinyi Zahera tayari ameanza kukisuka kikosi chake kwa kumsajili mshambuliaji chipukizi, Erick Msagati maarufu kwa jina la Lukaku. Nafasi alizopanga kuzifanyia kazi Zahera kwa ajili ya usajili ujao ni beki wa kati na pembeni, kiungo, winga na ushambuliaji. Mshambuliaji huyo aliyekuwa anaichezea timu ya U20 ya Yanga, wiki iliyopita aliweka rekodi ya kufunga mabao saba kati ya mechi tano alizozicheza

 

vijana iliyoandaliwa kwenye Uwanja wa JK Park jijini Dar es Salaam. Akizungumza na Spoti Xtra, Mratibu wa timu hiyo, Hafi dh Saleh alisema kuwa mshambuliaji huyo tayari amejiunga na timu hiyo juzi Jumatatu jioni huko Morogoro ilipoweka kambi kujiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Mtibwa. Saleh alisema, kocha Zahera ndiyo aliyewaomba viongozi wamsafi rishe kwenda Morogoro kwa ajili kwa lengo la kumuona zaidi baada ya kupata taarifa zake. Aliongeza kuwa, mshambuliaji huyo tayari ameongezwa kwenye usajili wa timu hiyo kati ya wachezaji sita waliopandishwa katika msimu huu akiwem

 

Godfrey ‘Boxer’ ambaye ni beki wa kulia tegemeo. “Lukaku amejiunga na timu baada ya kocha Zahera kupata taarifa zake ndiyo akamuita kambini,”alisema Hafi dh ambaye ni miongoni mwa wanachama waandamizi wa Yanga waliodumu na makocha wengi. “Kiukweli ni mchezaji mzuri mwenye kasi akiwa na mpira, pia uwezo wake mkubwa wa kufunga mabao aliokuwa nao ambao ameuonyesha kwa siku hizi mbili tukiwa huku kambini Morogoro kabla ya kuchukua maamuzi ya kumsajili,” alisema Hafi dh

Comments are closed.