The House of Favourite Newspapers

Kocha Yanga Awaondoa Wawili Kikosi Kitakachowavaa Kagera Leo

0

KOCHA Mkuu wa Yanga amechukua maamuzi ya kuwabakisha Jijini Dar es Salaam mabeki wake tegemeo nahodha Bakari Mwamnyeto na Ibrahim Hamad ‘Bacca’ kwa hofu ya kujitonyesha majeraha huku kiungo mkabaji Khalid Aucho akiungana na msafara wa timu hiyo, baada ya kumaliza adhabu ya michezo mitatu.

Kikosi cha Yanga jana alfajiri kilipanda Ndege kuelekea Mkoani Kagera kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara uaotarajiwa kupigwa leo Ijumaa saa kumi kamili jioni kwenye Uwanja wa Kaitaba.

Mwamnyeto na Bacca ni kati ya wachezaji waliokuwa wanaounda kikosi cha Timu ya taifa, Taifa Stars kilichocheza Fainali ya Mataifa Afrika (Afcon), mwaka huu zinazoendelea nchini Ivory Coast.

Akizugumza na Championi Ijumaa, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe alisema kuwa kikosi hicho kimesafiri kuelekea Kagera bila ya nyota watatu ambao ni Bacca, Mwamnyeto na Augustine Okrah kutokana na majeraha.

Kocha Gamondi

Kamwe aliongeza kuwa Bacca na Mwamnyeto walirejea nchini kutokea katika Afcon wakiwa na majeraha ambayo madaktari wa timu na kocha Gamondi wakashauri wabakie jijini Dar es Salaam kwa ajili ya vipimo zaidi huku wakiwa chini ya uangalizi.

Aliongeza kuwa licha ya kuwekwa chini ya uangalizi, lakini kocha ametoa mapumziko maalum kwa mabeki hao kwa hofu ya kujitonyesha huku mbeleni wakiwa na michezo migumu ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo muhimu kwao kupata ushindi.

“Kocha Gamondi ameona ugumu wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ambayo inawahitaji mabeki hao, hivyo akashauri ni bora wakapumzika huku wakiendelea na matibabu yatakayowarudisha mapema uwanjani.

“Hiyo ni baada ya kushauriana na Jopo la Madaktari wa timu hiyo, kabla ya kuchukua maamuzi ya kuwabakisha Jijini Dar es Salaam kuendelea na matibabu.

“Katika mchezo huu dhidi ya Kagera Sugar, Aucho anatarajiwa kuiongoza safu ya kiungo baada ya kumaliza kutumikia adhabu ya kufungiwa michezo mitatu ya ligi, ujio wake kutaimarisha kikosi chetu,” alisema Kamwe.

STORI NA WILBERT MOLANDI

”HUYU ni KIKOJOZI” – WAITARA AKICHAFUA HADI AKAPIGWA BUSU na MBUNGE MWENZAKE – FULL VICHEKO…

Leave A Reply