The House of Favourite Newspapers

Koeman Atupiwa Virago Barca

0

KLABU ya Barcelona  imemtimua kocha Mdachi, Ronald Koeman saa chache baada ya kupokea kichapo dhidi ya Rayo Vallecano jana usiku.

Taarifa za kufutwa kazi kwa Kocha huyo zimetolewa jana wakati Koeman na timu yake wakiwa kwenye ndege ya kurudi Barcelona kutokea kupokea kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Rayo Vallecano.

Barcelona ipo nafasi ya 9 katika Msimamo wa La liga na katika michuano ya Klabu Bingwa Ulaya imepoteza mechi zake mbili za kwanza katika hatua ya makundi kwa mara ya kwanza katika michuano hiyo.

 

Wakati huo Legend wa Klabu hiyo  Xavi Hernandez  anapigiwa chapuo la kubeba mikoba ya Mholanzi huyo katika viunga vya Camp Nou.

Leave A Reply