The House of Favourite Newspapers

Koffi Olomide Atiwa Mbaroni DRC

0

KOFFI (2)

Mwanamuziki nguli wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Koffi Olomide amekamatwa na polisi akiwa nyumbani kwake mjini Kinshasa.

Imeelezwa kuwa Koffi amekamatwa kwa agizo kutoka ofisi ya mwendesha mashtaka.

Staa huyo alikamatwa nchini Kenya Ijumaa iliyopita na kurudishwa DRC kesho yake asubuhi baada ya video yake kusambaa mitandaoni ikimuonesha akimpiga teke mmoja wa madansa wake aitwaye Pamela mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Jomo Kenyatta (JKIA) kwa ajili ya tamasha.

KOFFI (1)

Koffi akimpiga teke dansa wake.

Koffi anadaiwa kufanya tukio hilo baada ya Pamela kukorofishana na mwanamuziki wake aitwaye Cindy Le Couer anayedaiwa kuwa ni mpenzi wa Koffi.

Mbali na tukio hilo, mwanamuziki huyo alipoulizwa kwa nini alimpiga dansa wake alikana akidai kwamba alikuwa akimkinga na vibaka.

Kutokana na tukio hilo, Koffi alishindwa kutumbuiza mashabiki wake huko Bomas of Kenya baada ya tamasha hilo kuahirishwa.

Tukio hilo si la kwanza kwa staa huyo ambaye amekuwa akilalamikiwa kwa kuwapiga madansa wake, aliwahi pia kumpiga mpiga picha za habari na matukio mengine kama kashfa ya kuwabaka madansa wake.

Leave A Reply