Koletha aeleza alivyosahau gari baa

WAKATI wengi wakisahau vitu kama simu, funguo na vinginevyo kwa staa wa filamu za Kibongo, Koletha Raymond ametoa kali baada ya kueleza jinsi alivyosahau gari baa.  Koletha aliiambia Za Motomoto ya Risasi, kuwa siku hiyo alikwenda baa kunywa pombe akiwa na gari lake na ulipofika wakati wa kuondoka akasahau kama alikuja nalo.

“Sina hamu na pombe inaweza kukusahaulisha kila kitu. Siku hiyo nilisahau gari ikabidi nitafute la kukodi hadi nyumbani, asubuhi naamka ndiyo nikakumbuka nashukuru palikuwa salama,” alisema Koletha.


Loading...

Toa comment