The House of Favourite Newspapers

JPM: Nimewasamehe Makamba na Ngeleja – Video

  RAIS John Magufuli amesema amewasamehe wabunge January Makamba wa Bumbuli na William Ngeleja wa Sengerema kwa kile alichosema walimtukana kwenye simu.

 

Ameyasema hayo  katika mkutano wa wahandisi na wadau wa sekta ya ujenzi uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Septemba 4.

“Nakumbuka hivi karibuni kuna watu walinitukana na nikapata uhakika kwamba sauti zile ni zao, nikafikiria nikasema hawa wakipelekwa kwenye kamati ya siasa adhabu itakuwa kubwa. Walinitukana kwenye simu na nikahakikisha ni kweli ni sauti zao lakini nimewasamehe.

 

“Lakini wakajitokeza wawili wakaniomba msamaha,  nikasema nisipowasamehe nitabaki na maumivu makubwa sana.  Watu hao ni January Makamba na William Ngeleja nikaona niwasamehe tu.

“Waliomba msamaha nikasema ni vijana nimewasamehe. Kama palikuwa na mambo mabaya nyuma tuyasahau ili tukaanze upya maana kusamehe siyo jambo rahisi lakini saa nyingine inabidi usamehe,” amesema.

Comments are closed.