The House of Favourite Newspapers

Kortini Wakidaiwa Kuiba Mbolea ya Milioni 16.9 – Video

0

 

WATU tisa  kutoka mkoani Songwe wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka tisa likiwemo la kuiba mbolea yenye thamani ya TSh. Mil. 16.9.

 

 

Washitakiwa katika kesi hiyo ni Bashir Mfinanga (61), Siliak Mwaipopo (50), Juma Waziri (34), Juma Salehe (29), Zakaria Ndaya (40), Abas Sikanvika (34), God Mshana (30), Masumbuko Fumbo (43) na Zephania Kigola (33).

 

 

Washitakiwa hao kwa pamoja wamesomewa mashitaka yao na Wakili wa Serikali, Neema Mushi, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Yusto Ruboroga.

 

 

Mashtaka Makuu katika kesi hiyo ya jinai namba 15 ya mwaka 2021 ni kuiba mali iliyokuwa inasafirishwa pamoja na kukutwa na mbolea iliyopatikana isivyo halali. Katika mashtaka hayo inadaiwa kosa la kwanza hadi la tano liliwahusu washitakiwa Mfinanga, Mwaipopo, Waziri, Salehe na Ndaya.

 

 

Miongoni mwa washitakiwa hao, mshitakiwa Mfinanga anadaiwa kukutwa na mali ya wizi Oktoba 26, 2020 maeneo ya Tunduma Songwe ambapo alikutwa na mbolea kil.3007 aina ya AMMONIUM NITRATE ikiwa na thamani ya Sh. mil. 6.2 mali ya ORICA iliyokuwa inasafirishwa kutoka DSM kwenda Zambia.

 

 

Pia kosa la kukutwa na mbolea isivyo halali linamkabili mshitakiwa Sikanyika, Mshana, Fumbo Kigora. Katika kosa hilo, inadaiwa mshitakiwa Mshana, Desemba 12, 2020 alikutwa na Kilo 265.75 za Mbolea aina ya AMMONIUM NITRATE maeneo ya Tunduma mali ya ORICA.

 

 

Baada ya kusomewa mashtaka hayo washitakiwa wote walikana kutenda makosa hayo, hivyo upande wa Jamhuri umedai kuwa upelelezi bado haujakamilika, hivyo ukaomba iahirishwe hadi tarehe nyingine.

 

 

Hata hivyo washtakiwa hao wameshindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili wanaoàminika na bondi ya Sh. mil 5 kwa kila mdhamini, kesi hiyo imeahirishwa hadi keshokutwa Januari 28, 2021.

Leave A Reply