The House of Favourite Newspapers

Shigongo Ashiriki Mazishi ya Mama Yake Mkubwa

0

Mbunge Jimbo la Buchosa, Mhe. Eric Shigongo ameshiriki mazishi ya mama yake mkubwa, Bi. Agatha Kadikilo katika Kijiji cha Mwangika, Kata ya Bamgwe, Buchosa mapema jana Jumatatu, Januari 25, 2021.

Akizungumza katika msiba huo Shigongo amewasihi waombolezaji waliofika kujumuika ya familia yao katika mazishi hayo kuwa kifo ni somo kwa kila mtu kwani vitabu vya dini zote vinaeleza juu ya kifo hivyo ni vyema kila mtu akajiandaa kwa ajili ya siku yake ya mwisho kwa kufanya yaliyo mema.

“Maisha yetu hapa duniani ni mafupi sana, kila mmoja wetu ipo siku yake ataondoka, hivyo tunapaswa kumtumikia Mungu na kutomchukia mtu kwa sababu yeyote ile, sote tumeumbwa na Mungu kwa lengo moja tu la kumtukuza yeye huku tukitenda mema na kuwatendea mema wenzetu.

“Ni vyema wananchi wangu wa Buchosa tuwe tunashirikiana kwa kila Jambo ili kuimarisha umoja na ushirikiano wetu ili kuleta maendeleo ya Buchosa. Mama yetu Agatha apumzike kwa AMANI. AMEN…!” alisema Shigongo.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Leave A Reply