The House of Favourite Newspapers

Kortini kwa Tuhuma za Kuwaajiri Wageni Bila Vibali

0

 

Wafanyabiashara watatu wamefikishwa katika mahakama ya Wilaya Kinondoni jijini Dar es Salaam, kwa mashtaka manne likiwemo la kuwa ajiri raia wawili wa nchini China katika kampuni ya NASUTU TRADING CO.LTD bila kuwa na kibali cha kufanyia kazi nchini.

Washtakiwa hao ni Jenipha Munishi (29), Wun Chun (33)na Chen Xiao (25) ambapo wamefikishwa mahakamani hapo leo na kusomewa mashtaka na wakili wa Serikali, Shindai Michael mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Franko Kiswaga.

 

Akisoma hati ya mashtaka wakili Michael amedai kuwa, Februari 17, mwaka 2012 katika eneo la Ubungo Business Park mshitakiwa Jenipha akiwa Ofisa Mwajiri wa kampuni ya NASUTU TRADING Co. LTD anadaiwa kuwaajiri raia wawili wa kigeni kinyume cha sheria.

 

 

Imeelezwa kuwa, Februari 17 mwaka huu, mshitakiwa Chun na Xiao katika mda na wakati usiyojulikana eneo la Ubungo Business Park , washitakiwa hao walikutwa wakifanya kazi katika kampuni ya NASUTU TRADING CO.LTD bila kuwa na kibali cha kufanyia kazi.

 

Aidha, washitakiwa wote walikana tuhuma hizo na upande wa Jamhuri uliowakilishwa na wakili Michael umedai upelelezi umekamilika na kuomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwaajili ya kuwasomea maelekezo ya awali.

 

 

Naye Hakimu Kiswaga alisema dhamana ipo wazi kwa washitakiwa hao, ambapo walitakiwa kuwa na wadhamini wawili, wenye barua za utambulisho au barua kutoka kwa mwajiri na kusaini hati ya milioni 10.

 

 

Mbali na hapo, mshitakiwa wa pili na watatu ambao ni raia wa nchini China wao mahakama iliwaamuru kuwasilisha hati zao za kusafiria (Passport)mahakamani hapo.

 

 

Hata hivyo, mshitakiwa namba mbili na tatu ndiyo waliyokidhi masharti ya dhamana, huku mshitakiwa wa kwanza Jenipha alishindwa kutimiza masharti hayo na Hakimu Kiswaga alihairisha kesi hiyo hadi Machi 29, mwaka huu, na mshitakiwa Jenipha alipelekwa mahabusu.

 

Na Denis Mtima

 

Leave A Reply