The House of Favourite Newspapers

KUBENEA ADAI HUENDA BOMBARDIER ZIKAKAMATWA TENA – VIDEO

 

MBUNGE wa Ubungo – Dar es Salaam, Saed Kubenea akichangia hoja bungeni leo kuhusu Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano inayosimamiwa na Profesa Makame Mbarawa, ameomba ufafanuzi kutoka kwa Waziri Mbarawa akidai juu ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limefunguliwa kesi, London nchini Uingereza kutokana na deni la zaidi ya Tsh. Bilioni 100 hali ambayo amedai inaweza kusababisha ndege za Bombadier kukamatwa.

 

Hayo amesema leo Bungeni, Aprili 24, 2018, na kuongeza kuwa Waziri wa katiba na Sheria anafahamua suala hilo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali anafahamu, Asha Rose Migilo na viongozi wengine wanajua, tayari Serikali ya Tanzania imelipa malipo ya awali kwa mawakili kwa ajili ya kesi hiyo.

 

Mbunge huyo amesema nia ya Serikali ya kulifufua ATCL ni njema lakini inatakiwa kulisaidia shirika hilo kuondokana na mzigo wa madeni ili liweze kujiendesha kwa faida na kukuza uchumi wa Taifa.

 

VIDEO: MSIKIE KUBENEA AKIZUNGUMZA BUNGENI

Comments are closed.