The House of Favourite Newspapers

Kulazimisha uhusiano na mtu wa jinsia yako

0

married-gay-couple-121213
N
i kweli kabisa kwamba, kila mtu ana uhuru wa kuishi atakavyo bila kuvunja sheria za nchi. Hilo halina ubishi ndiyo maana kuna watu wanafanya mambo ya ajabu sana huko mtaani lakini kwa sababu hawajavuka mipaka ya sheria, tunawaangalia tu.

Wakati ukweli ukiwa hivyo, kuna jambo moja ambalo kwa kweli linanitia kinyaa tena sana tu. Hili ni lile la mwanaume na midevu yake kulazimisha kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwenzake, huu ni uungwana jamani?

t1larg.same.sex.marriage.ny.irptAchilia mbali hao, unakuta msichana mzuri anayestahili kuwa na mume wake lakini eti anamsifia msichana mwenzake na wakati mwingine kuchomekea ndogondogo kwamba anampenda, unajua anataka nini? Eti anataka kufanya mambo ya usagaji. Hili nalo ni tatizo kubwa sana.

Kwenye hii mitandao ya kijamii na simu za mkononi usumbufu huu umeshamiri mno. Unakuta mwanaume hata humjui, anakutumia picha yake kwenye mtandao akiwa kapozi kimahaba halafu anakuambia I love you. Au anakupigia simu, kukutumia sms na kukuambia eti anakupenda.

Jamani, dume zima na akili zako huoni aibu kumtaka mwanaume mwenzako kimapenzi? Hata kama umekazoea hako kamchezo, ndiyo kila mwanaume unayemuona umtamani? Unadhani kila mwanaume anapenda uchafu huo?

Huo siyo uungwana hata kidogo na wenye tabia hiyo waache mara moja kabla hatujaanza kuwashughulikia mmoja baada ya mwingine.

Juzi nilipata malalamiko kutoka kwa dada mmoja mwanafunzi wa chuo kimoja kilichopo jijini Dar. Huyu dada anasema kuna binti wanasoma na kuishi pamoja hosteli lakini amekuwa akimsumbua sana.

Mara ampe zawadi, mara ampigie simu na kumsifia kuwa ni mrembo. Wakati mwingine wakiwa chumbani anamshikashika kimahaba ndipo alipogundua kuwa, anamtaka kimapenzi.

 Huu ni upumbavu uliopitiliza, haiwezi kuleta picha nzuri hata siku moja kwa mwanamke kumtaka mwanamke mwenzake au mwanaume kumtaka mwanaume mwenzake na naomba niseme kuwa, kama una tabia hiyo ya kutongozatongoza watu wa jinsia yako, kaa mkao wa kuumbuka.

Ndiyo, hatuwezi kuvumilia hii hali, hatuwezi kuendelea kuwakalia kimya watu wachache wanaotaka kutuharibia jamii yetu iliyostaarabika. Mambo hayo yako huko nchi za watu wasio na maadili lakini kwetu Bongo siyo sawa kabisa. Mnakera sana nyie wenye tabia hiyo chafu.

Leave A Reply