The House of Favourite Newspapers

Kumbe! Wolper ana Mchumba Nje ya Nchi!

0

 

DAR: Staa mjasiriamali wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper Massawe, amesema siku atakayopagawa ndiyo atamposti mpenzi wake ambaye yupo nje ya nchi.

 

Wolper amesema yeye ni mmoja wa watu ambao wanalitangaza vyema Taifa kwa kuwa na mpenzi nje ya Nchi.

Ameliambia Gazeti la IJUMAA kuwa, ni kweli ana mpenzi mpya nje ya nchi ambaye huwa anawasiliana naye mara kwa mara na akimkumbuka huwa anamfuata huko aliko.

 

“Mnataka hadi muone tunaposti wapenzi wetu ndiyo mjue kama yupo?

“Sasa hivi nipo huru sana, naona kama nimezaliwa upya, nimebadilika sana ila siku nitakayopagawa, nitamposti, lakini kwa sasa bado sijapagawa na sijataka, mpenzi ni ninaye na tunawasiliana, unadhani nitakaaje sasa kwa kuwa yeye yupo mbali na hatuishi pamoja wala nchi moja?” Anahoji Wolper ambaye kwa sasa amejikita kwenye biashara ya nguo.

 

Aidha Jacqueline Wolper ameongeza kusema “Kutoishi naye pamoja kunafanya mara chache sana kuwa kimapenzi na sasa hivi nipo kikazi zaidi, nikimkumbuka nitaenda kumfuata au yeye atakuja naitangaza vizuri sana nchi”.

Stori: Imelda Mtema, Ijumaa

Leave A Reply