The House of Favourite Newspapers

Kumbukumbu ya Miaka Minne ya Kifo cha Baba Yake Shigongo Yafanyika Dar

0

20Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd, James Bukumbi enzi za uhai wake.

 

JANA ilitimia mwaka wa nne tangu kufariki kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd, James Bukumbi, ambapo ilifanyika  ibada fupi ya kumuombea.. Katika ibada hiyo  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Eric Shigongo, alitoa neno la nasaha kwa ndugu, jamaa na marafiki kwamba yatupasa kuwapenda wazazi wetu wakingali hai.

1.Mkurugenzi Mtendaji wa  Global Publishers Ltd, Eric Shigongo, akizungumza jambo.

Katika ibada hiyo iliyoambatana na misa ambayo ilihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwamo ndugu, marafiki na wafanyakazi wa kampuni hiyo, na ambayo ilifanyika nyumbani kwa mama mzazi wa Shigongo, huko Mikocheni, Mkurugenzi Mtendaji huyo alitoa nasaha hiyo kuhusu marehemu baba yake ambaye alizikwa kijijini Bupandwamhela Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.

2.…Akiendelea kuzungumza na watu waliohudhuria ibada hiyo.

Misa kama hiyo ilifanyika pia jana huko kijijini Bupandwamhela, Mwanza, ambako Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Masha Bukumbi, aliiwakilisha familia ya marehemu kuungana na wanakijiji wote katika kumkumbuka Mzee Bukumbi.

4.Mama yake Eric Shigongo aitwaye Asteria Kapera (aliyekaa kitini) wakati wa ibada.

Shigongo alisema hadi leo anamkumbuka baba yake kwa mambo mbalimbali aliyomfundisha  akingali mdogo, likiwemo suala la nidhamu katika masuala ya fedha, kuheshimu watu wa rika zote na kuthubutu kufanya jambo lolote ambalo baadaye litamletea mtu mafanikio.

3.Wajukuu wa marehemu Mzee James Bukumbi ambao wanajulikana kama  James ‘Mdogo’ (kulia) na James ‘Mkubwa’ wenye fulana nyeupe wakifuatilia ibada.

Alisisitiza kwamba kwa kiasi kikubwa zaidi mafanikio aliyo nayo yalitokana na elimu aliyoipata kutoka kwa baba yake ambapo alisema ataendelea kumuenzi na kufuata ushauri wake maisha yake yote.

5.Kulia kwa Mama Asteria ni Leah James Bukumbi na Lydia James Bukumbi (waliopo katikati) wakati wa ibada.

Naye dada yake Shigongo, Leah James Bukumbi,  alisema kuwa anawashukuru watu wote walioshiriki ibada hiyo fupi ya kumwombea baba yao tangu kufariki kwake na akasema siku zote za maisha yake atauenzi ukarimu wa baba yake, malezi mema ya uadilifu na kuwapeleka shule, mambo ambayo yamewafanya kuishi maisha ya furaha duniani.6.

Leah Bukumbi akizungumza jambo la shukurani kwa ndugu, jamaa na marafiki waliofika kwenye maadhimisho hayo.

Ibada hiyo ya kumbukumbu iliongozwa na Katibu wa Jumuiya ya Mtakatifu Augustino, Dominic Mushi, wa Parokia ya Mt. Martha Mikocheni B, akisaidiana na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Engelbert Lipambila.

7.Mjukuu wa marehemu Bukumbi, Deus James, akisoma risala ya marehemu kwa niaba ya familia.

Katika mafundisho yake jana, Mushi aliwaasa waumini kumweka Mungu mbele katika maisha yao ya kila siku na kutenda matendo mema, ambapo pia aliwatia moyo wana familia wa marehemu akisema kwamba yuko mahali salama na wazidi kumuombea.

8.Mjukuu mwingine wa marehemu aitwaye  Dkt. James akizungumza.

9.Mhariri mwandamizi wa Gazeti la Uwazi, Elvan Stambuli, akieleza  alivyomfahamu marehemu Bukumbi.     10..Katibu wa Jumuiya ya Mtakatifu Augustino, Dominic Mushi, wa Parokia ya Mt. Martha Mikocheni B akiendesha ibada. 11Shigongo na mkewe, Veneranda Ephraim wakati wa ibaada.12. 13 14

Sehemu ya wafanyakazi wa Global Publishers waliohudhuria ibaada hiyo.15 17

Mwenyekiti (kushoto) na Katibu wake wakijadiliana jambo.18 19  Ibaada ikiendelea.22Wajukuu wa marehemu

(PICHA: DENIS MTIMA)

Leave A Reply