The House of Favourite Newspapers

KIPINDI MAALUM GLOBAL TV KURUSHWA JUMAPILI MCHANA

0

NDUGU mfuatiliaji na mtazamaji wa Global TV Online, kufuatia wananchi wa Kijiji cha Kwakonje, Kata ya Kibindu Wilaya ya Bagamoyo, wapatao 1500 kumuomba Rais John Pombe Magufuli na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wawaokoe, baada ya nyumba zao zaidi ya 160 kuchomwa moto na kubomolewa na watu wasiojulikana, Jumamosi iliyopita.

Nyumba zilivyochomwa moto.

Global TV Online ilipanga kukuletea tukio hilo LIVE Jumamosi, Agosti 19, 2017 saa 1:00 jioni, lakini kutokana na maombi ya wakazi wa Kwakonje, wameomba kipindi hicho kirushwe Jumapili saa 8:00 Mchana.

Samahani kwa usumbufu uliojitokeza na tunakusihi usikose kuangalia Jumapili saa nane mchana.

SUBSCRIBE SASA ==> Global TV Online

Leave A Reply