The House of Favourite Newspapers

Kuna Tofauti Kubwa Kati ya Resume, Profile, CV, Biography na Autobiography

0

Kuna swali nimeulizwa na watu wengi sana na nimeona nilifafanue. Swali; Mbona CV yako ni ndefu sana kurasa 51 nani anasoma? Jibu; Kuna tofauti kubwa sana kati ya Resume, Profile, CV, Biography na Autobiography. Usichanganye! Kila moja ina kazi yake!

 

Usijeukaambiwa leta “CV” wewe ukapeleka “Resume” au ukaambiwa leta “Profile” wewe ukapeleka “Biography” au ukaambiwa una “Autobiography”? wewe ukafikiri ni “Biography”. Utakuwa umekosea maelekezo. Soma hichi ninachofafanua kwa makini na “forward” au “share” kwa wengine ili tusaidiane;

1. Resume; hii kwa “standard” haitakiwi kuzidi kurasa 2. Inatumika zaidi katika biashara na ajira. Ni “summary” ya ujuzi wako, uzoefu wako na stadi “skills” zako za msingi. “Resume” imetokana na neno la kifaransa linalomaanisha “summary”. Ni ufupisho wa CV yako!

 

Kazi ya “Resume” ni kumshawishi “mwajiri” au “mteja” akupe nafasi ya “usahili” au interview. “Resume” inatakiwa kuwa “targeted” au “customised” sio general. Lazima ui “review” kila unapoitumia kulingana na unakoipeleka.

2. Profile; hii kwa “standard” haitakiwi izidi nusu ukurasa. Hata ikiwa “paragraph” moja au mbili inatosha. Kazi ya “profile” ni kuonyesha “what you can offer” au “value proposition” au “unique selling proposition” yaani nini unaweza kufanya. Neno “profile” maana yake ni “outline”. Ndio maana “Profile” yako inatakiwa kuwa fupi sana kuliko “Resume” yako!

Mfano ukialikwa kuwa mgeni rasmi sehemu hawasomi “CV” wala “Resume” wala “Biography” yako wanasoma “Profile yako”. Profile yako haitakiwi kubadilika badilika yaani “customized” kila wakati kwa sababu ndio “personal brand” yako. “Brand” inatakiwa kuwa “consistent”. Ni kama “logo” ya bidhaa.

 

3. CV; Cv ni rekodi yako ya elimu na mambo mengine yote yanayokupa mamlaka au “authority” au kukubalika “credibility” katika eneo fulani kutokana na uliyofuzu katika fani yako “credentials” iwe ni kwenye “career” au “biashara” au “uongozi”. CV imetokana na neno la kilatini au “kirumi” ikimaanisha “the course of my life” ndio maana ni “ndefu”

 

Cv inatumika hasa katika “academic record” research “utafiti” “kazi za kitaalam” au “consultancy”, katika uteuzi wa nafasi mbalimbali za kitaasisi, kitaifa na kidunia “appointments”, katika uchunguzi wa sifa za mtu nk. CV haina wigo inaweza hata ikawa kurasa 50 inategemea umesheheni ujuzi kiasi gani.

 

CV haibadilishwi ila inaongezeka kulingana na ukuaji wako katika taaluma au fani yako. Kila unapofuzu au kupata ujuzi mpya au kuongeza elimu au kutunukiwa tuzo au weredi au uteuzi na CV yako pia inaongezeka. Kwa hiyo anayetaka kukujua kwa undani hakuombi “Resume” au “Profile” anakuomba CV.

4. Biography; Biography ni maelezo kuhusu maisha yako kama yalivyoandikwa na mtu au watu. Autobiography ni maelezo kuhusu maisha yako kama ulivyoandika wewe. Neno “Biography” limetokana na neno la kigiriki “bios” linalomaanisha “maisha”.

 

Mara nyingi “Biography” na “Autobiography” zinatumika katika kueleza “legacy” yako ya maisha iwe bado unaishi au umetangulia mbele za haki. Ndio maana kwenye “Biography” au “Autobiography” unaruhusiwa kueleza hata maisha yako ya ndani wewe, ndugu zako, jamaa na marafiki zako.

 

Yote haya nimeandika na kuyaeleza kwa undani sana kwenye “section” ya Career katika www.paulmashauri.com. Nimejitahidi sana kueleza kuhusu “job search”, “Cv, Resume, Profile, Biography, Autobiography”, Career Development, Career Change na Career Switch. Ukitaka kuyajua zaidi weka email yako tutawasiliana na wewe-Paul R.K Mashauri

Na Paul R.K Mashauri

Leave A Reply