The House of Favourite Newspapers

Breaking: Wanane Wafariki Ajalini Muleba, Kagera

0

WATU wanane, akiwemo mtoto mwenye umri wa mwezi mmoja ambaye mama yake amenusurika, wamepoteza maisha mkoani Kagera na wanne hali zao ni mahututi baada ya gari liitwalo Sabuni Express lenye namba za usajili T 392 AZB lililokuwa likielekea jijini Mwanza kupata ajali na kupinduka wakati likitoka eneo la Nshamba lililoko wilayani Muleba.

Akizungumza akiwa kwenye eneo la tukio,  Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kagera, Kamishina Msaidizi Revocatus Malimi, ametembelea majeruhi waliolazwa katika Hospitali Teule ya Rubya na Hospitali ya Ndolage na kusema kuwa katika ajali hiyo watu 23 walipata majeraha  madogo.

 

Leave A Reply