The House of Favourite Newspapers

Kushindwa Kujieleza kwa Wagonjwa kwa Madaktari Kwaleta Madhara kwa Afya Zao

0
Wagonjwa wameaswa kuwa wawazi kwa madaktari ili wapate matibabu sahihi

DAKTARI Mloganzila-Innocent Tesha kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili amesema kuwa baadhi ya wagonjwa wanashindwa kueleza kwa usahihi matatizo yao jambo linalohatarisha afaya zao.

 

Amesema kuwa baadhi ya wagonjwa wakifika kwa Daktari wanashindwa kujieleza kwa usahihi kuhusu magonjwa yao hivyo kusababisha madakatari kuwapataia dawa ambazo haziendani na matatizo yao, mfano amesema mgonjwa anaweza kuwa kuwa ana HIV lakini akaficha na kusema kuwa anaumwa kifua jambo ambalo linaweza sababisha kutopatiwa ufumbuzi sahihi wa tatizo.

Daktari na Mgonjwa

Naye daktari Ford Chisongela kutoka Hafford Health Clinic ya wilaya ya Temeke amewataka wagonjwa kuwa wakweli na kutoa maelezo sahihi wakati wanapoenda kujieleza kwa Daktari, ili kuweza kepusha matatizo ya kucheleweshwa kwa wagonjwa wengine kupatiwa huduma na kutopata tiba saahihi ambapo huatarisha afya zao.

 

Naye mtaalamu wa saikolojia Ramadhani Masenga, amesema baadhi ya watu hupenda kutafuta hadhi kwa kujilinganisha na watu fulani kwenye jamii, hivyo wakienda kwa daktari wanaeleza matatizo yao kwa kujilinganisha na watu fulani hii huwachanganya Madaktari na kushindwa kuwapatia dawa sahihi.

Leave A Reply