The House of Favourite Newspapers

KUTANA NA KIBIBI WANGARI FUNDI RADIO ZA MAGARI WA KENYA

KIBIBI Cecilia Wangari Kiminda wa Kenya bado yuko ‘ngangari’ dhidi ya umri wake,  akitengeneza radio zenye matatizo zilizoko katika magari.

Wangari ambaye ana karakana yake iitwayo Shosh Sounds,  aliliambia shirika la utangazaji la BBC Africa  kwamba anaipenda kazi yake hiyo na akaongeza kwamba:

“Naipenda kazi hii na familia yangu inaipenda.  Kila apendaye muziki anapenda kuishi maisha mazuri.  Ninapozungumza na watu huwa nafurahi,” anasema na kuongeza kwamba kufanya kazi kunahuisha maisha ya mtu na kwamba kazi ni muhimu ili kuondoa umaskini.

Comments are closed.