The House of Favourite Newspapers

KUZIBA NA KUVIMBA MIRIJA YA UZAZI (HYDROSALPINX)

HDROSALPINX’ ni hali ambayo mirija ya uzazi ya mwanamke inakuwa inavimba kwa kujaa majimaji na inaziba upande wa mwishoni mwa mirija. Mirija hii inapovimba huwa na uvimbe kama soseji, uvimbaji huu wa mirija na kuziba huwa wa pande zote mbili, kulia na kushoto. 

 

 Tatizo hili la kuvimba na kuziba kwa mirija husababisha ugumba kwa mwanamke. Pamoja na kujaa maji pia mirija inaweza kujaa usaha au damu. Tatizo hili huweza kumfanya mwanamke apoteze uwezo wa kuzaa yaani kuwa mgumba. Chanzo kikuu cha hali hii ni maambukizi katika viungo vya uzazi, ‘Pelvic Inflammatory Disease’ au kwa kifupi ni ‘PID’.

 

Maambukizi haya hupanda taratibu na huanzia ukeni. Kwa hiyo mwanamke anayesumbuliwa na tatizo la maambukizi ya mara kwa mara ukeni ni vema atibiwe vinginevyo baadaye anaweza kujikuta anashindwa kupata ujauzito.

Dalili za maambukizi ya mara kwa mara ukeni ambayo yanaweza kukufanya ukose uwezo wa kuzaa kwa kupata tatizo hili ni kutokwa na uchafu au majimaji ukeni yenye harufu mbaya na muwasho, maumivu ukeni, maumivu wakati wa kujamiiana na kuhisi uvimbe ukeni kama gololi. Ingawa siyo kila maambukizi ya kizazi husababisha kuziba mirija, bali endapo mwanamke atawahi hospitali na kupata tiba sahihi anaweza kupona na asiwe mgumba.

 

Mwanamke mwenye tatizo hili hutokea mirija inapoharibika maana yake yai haliwezi kuchukuliwa na kuingizwa katika mirija ya mbegu za kiume kwani haliwezi kupenya. Matatizo mengine yanayosababisha mirija ya uzazi ya mwanamke kuziba ni makovu kutokana na upasuaji wa awali wa kizazi au mirija, tabaka la ndani la kizazi kuwa nje ya kizazi na saratani ya mirija ya uzazi au vifuko vya mayai.

 

DALILI ZA TATIZO

Kwa jumla dalili hutofautiana kati ya mwanamke na mwanamke, lakini zipo dalili kuu za ugonjwa. Mgonjwa mwenye tatizo hili hulalamika maumivu ya mara kwa mara ya tumbo chini ya kitovu na husambaa katika nyonga zote na kiuno, wapo wengine hawaoneshi dalili zozote ila wakipimwa ‘Ultrasoud’ au ‘HSG’ huambiwa mirija imevimba au imejaa usaha.

 

Mwanamke hulalamika kutoshika mimba kwa zaidi ya mwaka tangu aanze kutafuta, tumbo kuuma mara kwa mara hasa anapokuwa katika siku zake za hedhi, mzunguko wa hedhi huvurugika na kutoona ute wa uzazi, kupoteza hamu na raha ya tendo la ndoa, ingawa mwanaume akipimwa mbegu za uzazi huwa vizuri.

UCHUNGUZI NA TIBA

Uchunguzi hufanyika katika kliniki za madaktari bingwa wa kina mama katika hospitali za mikoa na daktari akigundua tatizo atakupa dawa stahiki.

Comments are closed.