The House of Favourite Newspapers

Kwa mziki huu! Mkitoka mkatambike

0

DSC_0074Wachezaji wa Yanga Niyonzima na Tambwe wakishangilia.

Waandishi Wetu, Dar es Salaam
RAPA wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego katika moja ya mashairi ya wimbo wake anasikika akighani: “Najisikia kuwachana” kisha kuna watu wanaitikia: “Wachaneee!”

Sasa mashabiki na wadau wote wa soka wanatarajiwa kushuhudia kipute cha timu kubwa katika soka nchini, Simba na Yanga, kesho Jumamosi ambapo kipa upande umekuwa ukijinadi kuwa utawachanachana wapinzani.
Ni jambo la kawaida kwa mechi ya wapinzani hao kuwa na presha lakini safari hii presha inaonekana kuwa kubwa zaidi kwa kuwa ubora wa wachezaji hautofautiani kwa kiwango cha juu na kila upande umeonyesha lazima upate ushindi, kinyume na hapo basi ujue litaibuka la kuibuka.

IMG_5624

Wachezaji wa Ibrahimu Ajibu na Juuko Murshid (kulia) wakishangilia.

Mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara itapigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, ambapo Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 45 katika michezo 19, Yanga inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 43 katika mechi 18.

Kocha Simba amtaja anayemhofia
Kocha wa Simba, Jackson Mayanja, raia wa Uganda, amemtaja winga wa Yanga, Simon Msuva ndiye anayemhofia kuelekea katika mchezo huo.
Kauli hiyo inaweza kuwashangaza wengi kwa kuwa Amissi Tambwe na Donald Ngoma ndiyo washambuliaji wa Yanga ambao wameonekana kuwa na makali zaidi, lakini Mayanja yeye amemtazama Msuva katika jicho la tofauti.

Wachezaji wa Simba,(kutoka kushoto), Hassan Isihaka,(wa pili kushoto) Haji Ugando,Mwinyi Kazimoto,Ibrahimu Ajabu wakimpongeza,Hamis Kiiza(kushoto) baada ya kufunga moja ya mabao dhidi ya timu ya Mgambo Shooting mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam jana. Simba ilishinda mabao 5-1.(Picha na Yusuf Badi)

Wachezaji wa Simba,(kutoka kushoto), Hassan Isihaka,(wa pili kushoto) Haji Ugando, Mwinyi Kazimoto, Ibrahimu Ajibu wakimpongeza, Hamis Kiiza(kushoto) baada ya kufunga moja ya mabao dhidi ya timu ya Mgambo Shooting mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam jana. Simba ilishinda mabao 5-1.(Picha na Yusuf Badi).

Akizungumza na Championi Ijumaa, Mayanja kutoka katika kambi ya Simba mkoani Morogoro, alisema: “Msuva ndiye mwenye madhara na anayehitaji umakini katika kumchunga. Nimewaona Yanga katika mechi kadhaa wametumia mawinga kupeleka mashambulizi.
“Nitahakikisha mawinga wao hawapati nafasi ya kupiga krosi kwa washambuliaji. Najua (Deus) Kaseke naye ni hatari lakini Msuva ndiye hatari zaidi.”

Madee kumbe Yanga damu
Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Hamad Ali ‘Madee’, amejinadi kuwa kikosi cha Yanga ambacho yeye anakishabikia kipo fiti idara zote na haoni kama Simba wanaweza kukwepa kupata kipigo.
“Ninajiamini tena sana, Simba atapigwa tu. Sawa, siku za karibuni wameonekana kuwa vizuri lakini bado Yanga ina kikosi bora.

IMG_1161Wachezaji wa Yanga, Ngoma (kushoto) na Kamusoko (kulia).

“Mbele ukutane na Tambwe, Ngoma na Msuva ambao muda wote wana njaa ya mabao, kati tunao kina Niyo na Kamusoko, Simba watatokaje?” alihoji Madee na kuongeza:
“Pamoja na hivyo, bado namhofia Kiiza. Jamaa anajua na ninamkubali tangu akiwa Yanga na mpaka sasa bado namfuatilia kwa ukaribu.”

Kavumbagu: Yanga watakaa
Straika wa Azam, Mrundi, Didier Kavumbagu, aliyewahi kukipiga Yanga, naye amefunguka kuelekea mchezo huo kwa kusema:
“Nafahamu mechi za Yanga na Simba hazitabiriki lakini hii ya Jumamosi naona Simba ina asilimia kubwa ya kushinda. Simba wanajiamini kwa kuwa wameshinda mechi sita mfululizo lakini pia kocha wao ni mtu anayelijulia sana soka la Afrika Mashariki.”
“Mayanja ataisumbua sana Yanga, namfuatilia tangu akiwa Rwanda, Uganda, Kenya na hata Kagera Sugar alikuwa na timu ndogo lakini alikuwa msumbufu sana.”
Kwa kuwa katika mchezo uliopita baina ya vigogo hao Yanga ilishinda mabao 2-0 wafungaji wakiwa ni Amissi Tambwe na Malimi Busungu katika dakika ya 44 na 79, wawili hao wamejinadi kurudia walichokifanya Septemba 26, 2015.
“Tumejipanga kuhakikisha tunaibuka na ushindi siku hiyo lakini natamani sana nirudie rekodi kama iliyopita ya kuifunga Simba katika dakika ya 79,” alisema Busungu.
Upande wa Tambwe alisema: “Mechi itakuwa ngumu lakini kabla kipindi cha kwanza hakijamalizika, tunatakiwa kuwamaliza kama ilivyokuwa mwanzo, namuomba Mungu anijalie hilo.”

Kurejea Dar
Katika kambi ya Simba iliyopo Morogoro, habari ni kuwa wachezaji wote wapo fiti na madai kuwa Abdi Banda aliumia mazoezini imeelezwa kuwa siyo kweli kwa kuwa mpaka jana jioni alionekana akiwa fiti pamoja na wenzake.
Yanga ambao wapo Pemba kwa ajili ya kambi ya mchezo huo, wao wanaweza kumkosa nahodha wao, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ambaye hajawa fiti lakini timu zote zimekuwa zikificha juu ya kurejea Dar. Imeelezwa kuwa Simba walitarajiwa kurejea jana usiku huku Yanga wakitua leo Ijumaa kwa ndege ya kukodi mida ya mchana.

Waandishi: Wilbert Molandi, Nicodemus Jonas, Hans Mloli na Sweetbert Lukonge

Leave A Reply