The House of Favourite Newspapers

Kwa nini mimi tu niteswe na mapenzi kila siku?

0

lonely-girl-sitting-on-the-stairs-4023

Na Gabriel Ng’osha

Mpenzi msomaji wa XXLove ni Jumatatu nyingine murua tunakutana hapa jamvini kujadili juu ya maisha ya uhusiano. Kutoka pale tulipoishia wiki iliyopita, wiki hii tunaendelea na sehemu ya pili ya mada hii ya Kwa Nini Mimi Tu Niteswe na Mapenzi? Endelea…

HIVI ulishawahi kujiuliza kwamba, tangu umeanza kutafuta kazi, umepata kazi ngapi na mwisho wa siku kazi hizo ukaziacha ama ukaachishwa au mkataba wako ukafika mwisho?
Kama ilivyo hali ya kutafuta au kupata kazi inayokufaa, ndivyo ilivyo kwenye uhusiano wa kimapenzi katika kumpata mwanaume au mwanamke anayekufaa.

Angalizo; simaanishi uwe unachepuka na kila mtu ili umpate anayekufaa, la hasha! Najua ukifanya hivyo utaangukia pua.

Ninachomaanisha ni kwamba, unapaswa kupata muda wa kumsoma mtu kama anakufaa kwa kumfuatilia, kumchunguza na kuangalia nyendo zake.

Kumpata mpenzi wa kweli au wa dhati ni safari ndefu ambayo inahitaji utashi wa hali ya juu wenye kumuomba na kumshirikisha sana Mungu katika kupata mtu sahihi.

Usihuzunike kwa sababu wewe siyo wa kwanza kuumizwa na si jambo la kawaida kuwa kwenye uhusiano bila kuumizwa, japokuwa maumivu yanatofautiana kati ya mtu na mtu.

Wengine wamekuwa wakiumizwa na vijitabia vidogovidogo na vya ajabu vya wapenzi wao kama uongo, utapeli, usengenyaji, gubu, visirani, uchoyo na kadhalika.

Kila kitu kwenye maisha kina maumivu, iwe masomo, mpira na hata muziki au mitindo kwani ili kufikia hadhi ya kimataifa lazima utapitia misukosuko, kejeli, manyanyaso, maumivu, majonzi na hata kukosa furaha. Lakini kama ukikomaa, hatimaye utaibuka mshindi. Wapo wapenzi wengi wamekuwa wakilia na
kunung’unika, wakijiona wakosaji kwa sababu ya maumivu ya kila mara katika uhusiano wao.

Usilalamike na kujiona mpweke katika maisha yako kwa kuwa mpenzi wako wa kwanza alikuacha, wa pili
mkakosana, wa tatu mkaachana na wa nne juzikati alifariki dunia. Pole!
Kaa ukijua hata kwenye mapenzi kuna milima, mabonde, mito, jangwa na vitu vingine vinavyoonekana na
visivyoonekana.

Wakati mwingine mapenzi ni maumivu, tena maumivu makali hasa, yanauma, yanakera, yanatesa na hata kukatisha tamaa ya kuishi, hasa kwa mtu uliyempenda kwa dhati na kumuamini, uliyemkabidhi moyo wako aulinde na kuutunza lakini thamani yako akaitupa kule kwa kukutesa na kukutenda vilivyo.

Kama kuna kitu kinachowatesa wanadamu wengi, basi ni mapenzi na kama kuna kitu kinachoumiza zaidi katika maisha ya mwanadamu huyohuyo
bila shaka ni mapenzi. Weka akilini mwako kuwa maumivu ni sehemu ya maisha ya mwanadamu.

KUFAHAMU YOTE HAYA NA MENGINE, NUNUA GAZETI LA IJUMAA WIKIENDA, LEO April 25, 2016

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz

Leave A Reply