The House of Favourite Newspapers

Wafungwa 293 Waachiwa Ukonga, Keko, Segerea, Wazo Hill – Dar

0

JUMLA ya wafungwa 293 kutoka magereza ya Ukonga, Keko, Segerea na Wazo Hill jijini Dar es Salaam jana wameachiwa huru kwa msamaha wa Rais  John Magufuli alioutoa kwa wafungwa 5,533 waliokuwa wakitumikia kifungo kwenye magereza mbalimbali nchini.

Wafungwa hao waliachiliwa huru jana Desemba 10, 2019 Mbele ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam,. Abubakar Kunenge, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam ambapo kwa pamoja wamewataka walioachiliwa huru kwa msamaha huo kuhakikisha hawarudii kufanya makosa.

Naye Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishina Msaidizi wa Magereza, Julius Mtambala, amesema kati ya wafungwa hao 293 walioachiliwa,  130 wanatoka Gereza la Ukonga, 54 Gereza la Keko, 74 Gereza la Segerea na 35 wanatoka Gereza la Wazo Hill.

 

Leave A Reply