#GlobalMusic: Kwenye Rotation Yako Weekend Hii, Iweke Na Hii ‘Sweet Love’ Ya Heri Muziki – (Audio)

Bado nazidi kuzisogeza kwako kali za kuwa nazo weekend hii kwenye rotation ya playlist yako. Its Saturday ya March 04 2017 na leo shavu la midundo linaenda kwa msanii kutoka Bongo Flevani, Heri Muziki.

Heri Muziki amerudi tena kuiteka attention yako  na kazi yake mpya iitwayo ‘Sweet Love’. Ndani ya wimbo huu, Heri Muziki anatusimulia love story kati yake na somebody special, anaendelea kuusifia uzuri wake na kuweka wazi hisia zake kwa mtu huyo, akitaka ajue kuwa hata wakiongea vipi kwake amezizi amedoro

Hadithi ya pendo nataka nikueleze, nataka nikupe pendo nilikoleze, sina mwingine wa kusema nae, kama ni mapenzi nitabaki nae…./ we ndio my sweet, sweet love penzi lako nimesizi me nimedoro….“- Heri Muziki anaimba.

 Producer wa mdundo huu anitwa Bacteria huku mixing and mastering vikisukwa na mkali Tiddy Hotter.

Bonyeza Play kusikiliza ‘Sweet Love’ hapa chini, feel free pia kui-download ili ikae karibu yako weekend nzima.

Heri Muziki – Sweet Love (Official Audio Release)

 

Imeandikwa Na: Sandra Brown

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, muziki na nyingine zikufikie kwa wakati.

Loading...

Toa comment