The House of Favourite Newspapers

KWESE SPORTS WAUNGANA NA TBC KUONYESHA KOMBE LA DUNIA

Mkurugenzi wa Kwese Free Sports Tanzania (KFS), Joseph Sayi,  akiongea na wanahabari katika ofizi za TBC Mikocheni jijini Dar.
Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt Ayoub Rioba.
Mkurugenzi wa Kwese Free Sports Tanzania (KFS), Joseph Sayi (kushoto) akiwa na Dkt Ayoub Rioba na Sayi wakisaini mkataba wa ushirikiano wa kuonyesha Kombe la Dunia.
Wakiuonyesha mkataba.

KAMPUNI ya Kwese Free Sport (KFS) imeingia mkataba na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kwa ajili ya kurusha matangazo ya Kombe la Dunia bure linalotarajiwa kuanza Juni, mwaka huu nchini Urusi.

 

Michuano hiyo itakayodumu kwa takribani mwezi mmoja, itakuwa inarushwa na chaneli za TBC 1, TV 1 na TBC Taifa ambazo zote zinapatikana katika king’amuzi cha StarTimes.

 

Mkataba huo umesainiwa na wakurugenzi wa mashirika hayo katika ofisi za TBC zilizopo Mikocheni, Dar es Salaam ambapo kwa upande wa TBC alikuwepo Dr Ayoub Rioba na upande wa KFS ni Joseph Sayi.

 

Sayi alisema kuwa wameingia mkataba huo lengo likiwa ni kuwapa burudani watazamaji wa soka kipindi chote cha michuano hiyo.

 

“Tumeingia mkataba KFS na TBC kwa ajili ya kurusha matangazo ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 na lengo ni kutoa burudani kwa watazamaji wetu kipindi chote cha michuano hii,” alisema.

 

(PICHA; MARTHA MBOMA | GLOBAL PUBLISHERS)

Comments are closed.