The House of Favourite Newspapers

Lake Oil Mdhamini Mkuu Tuzo Za Chaguo La Mlaji Afrika 2023

0
Mwanzilishi wa Tuzo za Chagua la Mlaji Afrika (CCAA) Diana Laizer (wa pili kulia) akipeana mkono na mkurugenzi mtendaji wa Lake Oil Abdulrahman Mohamed (wa tatu kushoto) muda mfupi baada ya kampuni ya Lake Oil kutangazwa mdhamini mkuu wa CCAA 2023. Wanaoshuhudia ni wadhamini wengine, kushoto ni Furaha Mohamed kutoka Horizon Digital akifuatiwa na Azmina Mohamed kutoka mgahawa wa Samaki-Samaki na kulia ni Juma Nuru, mkurugenzi rasilimaliwatu wa Lake Oil.

Dar es Salaam 6 Julai 2023: Kampuni ya Lake Oil Tanzania, imetangazwa kuwa mdhamini mkuu wa Tuzo za Chagua la Mlaji Afrika(CCAA)  kwa mwaka huu wa 2023.

Ikiwa ni sehemu ya kusaidia walaji kutoa maoni yao juu ya ubora wa bidhaa na huduma wanazozipata sokoni, tuzo za CCAA mwaka huu zinatarajia kushindanisha makampuni mbalimbali katika tuzo zaidi ya aina 70.

Akizungumza katika hafla ya kuwatambulisha wadhamini ikiwemo mdhamini mkuu, Mkurugenzi Mtendaji wa CCAA Diana Laizer aliishukuru kampuni ya Lake Oil kwa kukubali kuwa mdhamini mkuu na kuyataka makampuni mengine yenye nia ya kudhamini kujitokeza.

“Kwaniaba ya CCAA napaenda kushukuru kampuni ya Lake Oil kwa kukubali kuwa mdhamini mkuu wa tuzo za CCAA kwa mwaka 2023. Udhamini wao unaonyesha namna ambavyo kampuni inatambua na kuunga mkono nafasi ya walaji au wateja kutoa maoni yao kwa bidhaa na huduma wanazozitumia,” alisema.

Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Lake Oil Tanzania Abdulrahman Mohamed (wa tatu kushoto) akiongea wakati wa hafla ya kutambulisha kampuni ya Lake Oil kama mdhamini mkuu wa Tuzo za Chagua la Mlaji Afrika 2023 (CCAA). Wengine ni wadhamini kushoto ni Furaha Mohamed kutoka Horizon Digital akifuatiwa na Mwanzilishi wa Tuzo za Chagua la Mlaji Afrika (CCAA) Diana Laizer. Wa kwanza kulia ni Azmina Mohamed kutoka mgahawa wa Samaki-Samaki akifuatiwa na JumaNuru, mkurugenzi rasilimaliwatu wa Lake Oil.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji waLake Oil Abdulrahman Mohamed alisema kampuni yake inajivunia kuwa sehemu ya wadhamini wa tuzo hizo ambazo imekuwa ikishiriki tangu zilipoanza.

“Tumekuwa tukishiriki katika tuzo hizi tangu zilipoanza. Kwetu sisi tuzo hizi zimetujenga sana kwakuwa zimetusaidia kupata mrejesho kutoka kwa watumiaji wa bidhaa zetu na kutupa nafasi ya kuboresha huduma na bidhaa zetu kulingana na wateja wanavyotaka,” alisema.

Azmina Mohamed ambaye ni meneja masoko wa mgahawa wa Samaki-Samaki ambao pia ni wadhamini wa tuzo hizo, alisema Samaki-Samaki wameamua kudhamini tuzo hizo kutokana na umuhimu wake.

“Tuzo hizi ni muhimu sana kwakuwa zinatoa mrejesho kwa watoa huduma na kwahiyo zinachochea utoaji wa huduma bora jambo ambalo linasaidia kukuza biashara. Sisi kama Samaki-Samaki tumeona ni jambo jema kuunga mkono tuzo hizi kutokana na umuhimu wake,” alisema.

Leave A Reply