The House of Favourite Newspapers

Lala salama Shinda Nyumba; Wasomaji wachangamkia kuponi

0

2Ofisa Masoko wa Global Publishers, Yohana Mkanda akimwelekeza Mkazi wa Bunju, Dar aitwaye Jelioni Mbogela.

3

Haji Rajab Mkazi wa Bunju akijaza kuponi.

4

Msomaji akiweka kuponi yake katika ndoo maalum ya Bahati Nasibu.

5

Litha Tadeus (kulia) akipewa maelekezo na Mkanda namna ya kujaza kuponi yake.

6

Mkanda (katikati) akizungumza na msomaji, Juliana Boyi (kushoto) baada ya kujaza kuponi yake. Kulia ni msomaji akilisoma gazeti lake.

7

Abdu Tangila akijaza kuponi kushiriki Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba.

8

Hamad Salim (kulia) akisaidiwa na Mkanda kujaza kuponi yake kuchangamkia Shinda Nyumba.

9

Joram Joseph akijaza kuponi kushiriki droo kubwa ya Shinda Nyumba.

10

Wasomaji mbalimbali wa Magazeti ya Global wakiwa na nakala ya gazeti kila mmoja eneo la Stendi ya Daladala ya Bunju.

11

Wasomaji wakiwa na magazeti yao.

NA DENIS MTIMA/GPL

ZIKIWA  zimesalia siku mbili tu kuchezeshwa kwa droo kubwa ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba, leo Jumatatu wasomaji wa Gazeti la Michezo la Championi na Ijumaa Wikienda wamechangamkia kununua kwa wingi na kushiriki kujaza kuponi zinazopatikana ndani ya magazeti hayo.

Maeneo yaliyotembelewa na kukuta wasomaji wa magazeti hayo wakihamasika kuyanunua na kushiriki droo hiyo ni Bunju, Mbezi na Tegeta jijini Dar es Salaam.

Bahati nasibu hiyo inaendeshwa na Kampuni ya Global Publishers wachapishaji wa Magazeti ya Championi, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Ijumaa Wikienda.

Akizungumza na wakazi wa eneo hilo, Ofisa Masoko wa Global Publishers,Yohana Mkanda alisema kuwa zimesalia siku mbili tu hivyo wachangamkie fursa hiyo kwani inaweza kuwa nyumba hiyo miongoni mwao.

Katika uhamasishaji huo, Yohana Mkanda alirudia wito wake kwamba: “Siku zimesalia mbili tu ambazo ni za lala salama hivyo nunueni Magazeti ya Global mengi na mjaze kuponi ili kujiongezea nafasi ya kushinda nyumba kwani unaweza kuwa wewe au yule na kugeuka baba au mama mwenye nyumba! Hivyo, fursa ndiyo hii, bahati humjia mtu yeyote, kwa hiyo nunua Magazeti Pendwa yaliyojaa bahati na kila namna kila wakati. Kazi kwako, nyumba ndiyo hiyoo…!!!”

Katika droo hiyo ya Shinda Nyumba inayosubiriwa kwa hamu na wasomaji wa magazeti hayo, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda ambapo itachezeshewa katika Viwanja vya Zakhem, Mbagala jijini Dar.

Leave A Reply