The House of Favourite Newspapers

Lava Lava Ammwagia Sifa Kiba

0

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva kunako lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Abdul Idd ‘Lavalava’ ameonesha kummwagia sifa bosi wa lebo ya King’s Music, Ali Salehe Kiba ‘King Kiba’.

 

Akizungumza na Risasi Vibes, Lavalava amesema kuwa, K iba ni msanii mkubwa anayefanya vizuri na anatambua nani ana kipaji na ndiyo sababu alisifia ngoma zake kuwa ni nzuri.

 

“Kiba ni msanii mkubwa sana na kusifia ngoma zangu nashukuru sana, kwa sababu yeye anatambua vipaji vya wasanii na kama ikitokea pande zote mbili kukubaliana, tunaweza kufanya kolabo,’’ alisema Lavalava.

 

Hiv i karibuni, Kiba alikaririwa kwenye moja ya vituo vya redio nchini akimsifia Lavalava kuwa ana nyimbo nzuri.

STORI | Happyness Masunga | Risasi

 

Leave A Reply