The House of Favourite Newspapers

LAVALAVA: Diamond Ana Mapungufu, Tunavumilia, Alikiba….! – Video

Hit maker wa ngoma ya Go Gaga, Lavalava kutoka WCB, ambaye usiku wa kuamkia leo ameachia video ya ngoma yake mpya, ‘Nitake Nini’ amefungukia furaha aliyonayo baada ya menejimenti yake kuandaa tamasha kubwa la Wasafi Festival linalotarajiwa kuanza Jumamosi hii, Novemba 24, 2018, akisema litatoa fursa kwa wasanii wengine wachanga kupata nafasi ya kuonesha vipaji vyao.

 

Lavalava amesema hayo wakati akifanya mahojiano na Global TV Online, Lavalava amesema bosi wao ambaye ni Diamond Platnumz ana mapungufu yake lakini wanavumilia akibainisha kwamba siyo rahisi kwa wasanii wa WCB kumpelekea kazi (ya muziki) Diamond akaiubali harakaharaka, lazima ataihaji ifanyiwe maboresho ili iendane na anachokiamini katika ushindani wa tasnia hiyo.

 

Aidha, Lavalava amefunguka kuwa ugumu wa WCB ni kwamba wana ushindani wa ndani kwa ndani (yaani wao kwa wao), na ushindani wa nje (kushindana na wasanii wengine wasio wa WCB) jambo ambalo linawafanya kukaza buti na kufanya kazi kwa bidii kubwa.

 

“Ukilegalega hata menejimenti itakushangaa, unaona kabisa Mbosso anajitahidi, kila mtu anaona, halafu wewe umekaa pale umebweteka? Uzuri ni kwamba ukifanya kazi nzuri hata mitandao inasema, mashabiki wanaona.

 

“Ugumu wa bosi wetu siyo mtu wa kukubali kitu kirahisi, unaweza kufanya verse ukampelekea lakini asikubali muda huo, kwa hiyo kuna tabu kidogo ya kumwelesha kwamba hiki kitu unakitaka, mpaka kukubali kitu anachokitaka inachukua muda sana, mwisho wa siku tunachukulia kama kazi.

 

“Kwa hiyo Diamond ana mapungufu yake lakini anatufundisha na kutuelimisha kwamba tusichukulie poa haya mambo siyo marahisi, hayaendi kiholela, so ni vitu ambavyo tunavumilia tu,” alisema Lavalava. 

 

Lavalava amefunguka pia kuhusu mwanamuziki Alikiba kupitia kinywaji chake cha Mofaya, ambapo ameamua kudhamini tamasha la Wasafi Festival ambapo amesema licha ya kutopata uhakika kama ni kweli, lakini ni jambo jema sana kibiashara na kushirikiana kama wasanii wa Tanzania kuinua tasnia hiyo.

VIDEO: MSIKIE LAVALAVA AKIFUNGUKA

Comments are closed.