The House of Favourite Newspapers

WASANII 15 BONGO WALIOKUZWA NA SANAA WAKANG’ARA KISIASA

Image result for SUGU
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’

SIASA hasa ya vyama vingi lazima ukubali kuwa na makundi mawili ya wanaokupenda na wanaokuchukia; utake usitake.  Kwenye sanaa makundi hayo mawili hayapo! Kilichopo ni ushabiki ambao hautengenezi uadui kupitia itikadi, dini, kabila, rangi na ukanda!

 

Ukiwa chama fulani cha siasa unakuwa umejipambanua kabisa kwamba wale wa upende mwingine wa siasa hamfungamani nao. Lakini kwenye sanaa, msanii akiwa MwanaHip Hop haimaanishi hatapata mashabiki wa Dansi vivyo hivyo hawezi kuwa adui kwa sababu haimbi Taarab. Hii ndiyo tofauti ya siasa na sanaa.

 

ULINGANIFU WA SANAA NA SIASA

Tabia moja kubwa inayoweza kuilinganisha Sanaa na Siasa ni kuwa; kazi hizi mbili zote zinategemea mtaji wa watu. Huwezi kushinda nafasi za uongozi wa kisiasa kama huna wafuasi wengi wanaokuunga mkono. Kadhalika huwezi kuwa msanii mkubwa bila kuwa na kundi kubwa linalosapoti kazi zako.

 

Kwa namna moja au nyingine ni rahisi siasa na sanaa kuichanganya na kupata matokeo chanya, kwa upande wowote mtu anaotaka kuufanikisha. Ingawa ni nadra kumuona mwanasiasa akiacha siasa na kuwa msanii lakini wengi wao wamekuwa wakiwatumia wasanii wakubwa kuwapa kura za kisiasa.

 

Mlango mkubwa ulio wazi ni wa wasanii kuingia kwenye siasa. Dunia nzima wameta pakaa wanasiasa wasanii ambao walitumia nguvu ya sanaa kuwavusha kuingia kwenye siasa. Mfano; Arnold Schwarzenegger ambaye alikuwa mcheza filamu lakini baadaye akawa Gavana wa Jimbo la Califonia nchini Marekani.

 

Mwingine ni kijana Robert Kyagulanyi Ssentamu, ‘Bob Wine’ mwanamuziki wa Uganda ambaye kwa sasa ni ni Mbunge wa Jimbo la Kyaddondo na mwingine ni Msanii Charles Njagua ‘Jaguar’ aliyeshinda ubunge katika Jimbo la Starehe nchini Kenya.

 

1 : SUGU

Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ni MwanaHip Hop maarufu Bongo. Alianza muziki kama sehemu ya kujitetea na hali yake duni kimaisha. Sanaa haikumwangusha, ikampa umaarufu kutokana na nyimbo kali alizotoa ambazo ni pamoja na Ni Mimi, Zaidi na Zaidi na Nje ya Bongo. Mtaji wa watu alioupata kwenye sanaa akautumia kunyakua Jimbo la Mbeya Mjini katika uchaguzi wa mwaka 2010.

Related image

2 : PROF. JAY

Ukirudisha hisia miaka ya 90 utakutana na nyimbo za msanii Joseph Haule ‘Prof. Jay zilizokuwa moto wa kuotea mbali. Kila sauti ya Prof. Jay iliposikika watu ‘walipagawa’, albamu kama Machozi Jasho na Damu vijana hawakuambiwa kitu zaidi ya kuipenda. Umaarufu wa sanaa alioupata Prof. Jay ndiyo uliokuwa mtaji wake hadi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mikumi.

 

3 : MARTHA MLATA

Nyota yake ilianza kung’ara katika sanaa, zamani akiimba zaidi nyimbo za dini. Huyu si mwingine ni mwanamama Martha Mlata ambaye baadaye alitumia umaarufu alioupata kwenye sanaa kuingia kwenye siasa, ambako hakukwama kuupata Ubunge wa Viti Maalum CCM kutoka Mkoa wa Singida na baadaye kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wa mkoa.

Image result for JOKATE

4 : JOKATE

Jokate Mwegelo, awali alipitia kwenye mashindano ya urembo, akashiriki Shindano la Miss Tanzania 2006 na kushika namba 2, umaarufu wake ukaanza kuchipuka. Hakuishia hapo, akajitosa kwenye muziki na filamu. Fani hizo zikazidi kumpa nguvu na ndipo alipoingia kwenye siasa ndani ya CCM akatumika kama mhamasishaji vijana, alipokubalika huko mwenyekiti wa chama ambaye ni rais John Magufuli akamteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe.

Image result for Hadija Shabani ‘Keisha

5 : KEISHA

Wimbo wa Uvumilivu alioimba msanii Hadija Shabani ‘Keisha’ ulimpatia wafuasi wengi. Licha ya hali yake ya ulemavu wa ngozi ‘albino’ hakuuacha umaarufu wake alioupata unyauke. Alijikita kwenye siasa ambako kwa sasa anakula maisha ndani ya CCM akiwa kama Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya chama hicho tawala, nafasi ambayo ni nyeti katika siasa.

Image result for mkubwa fella

6 : FELLA

Wengi wamemfahamu Said Fella kupitia muziki na hasa uongozi wa Kundi la TMK Wanaume Family. Miaka yote amekuwa mtu wa sanaa, hata kama haimbi lakini ni muhimili wa wasanii wengi, hiki ndicho ‘kinachombeba’ kwenye jamii. Mwaka 2015, aligombea Udiwani Kata ya Kilungule jijini Dar akashinda, lakini kilichomsaidia kuvuka ni umaarufu alioupata kwenye sanaa.

Related image

8 : UWOYA

Irene Uwoya alishika nafasi ya kwanza kura za maoni viti maalum mkoani Tabora kuwakilisha vijana ndani ya CCM, hakuwa mbunge kwa sababu kura za urais hazikumpa sifa, lakini mafanikio haya aliyapata baada ya kuutumia mtaji wa watu alioukusanya kutoka kwenye mashindano ya Miss Tanzania 2006 aliposhika nafasi ya 3 na kwenye fani ya uigizaji.

Image result for wema sepetu

8 : WEMA

Wengi wanamtazama kama msichana asiyejitambua na asiyekuwa na bahati kutokana na tuhuma mbalimbali za kijinai zinazomkabili. Ni Miss Tanzania 2006, ana mtaji mkubwa sana wa watu, aliotoka nao kwenye mitindo na filamu. Umaarufu huo ndiyo uliompa nguvu ya kwenda Singida kutafuta nafasi ya ubunge ndani ya CCM. Hakubahatika kupenya kwenye kura za maoni lakini alionesha upinzani mkubwa kwa wagombea wenzake.

 

9 : KINGWENDU

Uingizaji, hasa fani ya uchekeshaji ilimng’arisha kisiasa msanii Rashid Mwinshehe alipoamua kujitosa kutafuta ubunge katika Jimbo la Kisarawe. Kampeni zake zilijaa sanaa ya vichekesho na chupuchupu ashinde kupitia chama cha Cuf kwenye uchaguzi wa mwaka 2015.

Image result for afande sele CHADEMA

10 : AFANDE SELE

Mfalme wa Vina Bongo, Seleman Msindi ‘Mtoto wa Morogoro’. Sanaa imempa ustaa. Mwaka 2015 akajitosa kwenye siasa akitaka ubunge wa Morogoro mjini kupitia chama cha ACT – Wazalendo, hata kama hakupata lakini alifanya vyema kisiasa.

Image result for MWAKIFWAMBA

11 : MWAKIFWAMBA

Ni Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, huyu si mwingine ni Simon Mwakifwamba ambaye nyota yake alichomoza kupitia fani ya uigizaji. Leo hii ndiye Katibu Mwenezi wa Mkoa wa Dar es Salaam, nafasi ambayo ukimuuliza hata yeye atakuambia kuwa imetokana na kazi yake ya sanaa.

 

12 : MR SIMPLE

Anaitwa Renatus Pamba, alivuma kupitia kazi ya muziki baadaye aligombea udiwani Kata ya Sinza mwaka 2010 na kushinda.

Image result for BABA LEVO

13 : BABA LEVO

Crayton Revokatus ‘Baba Levo ni mwigizaji maarufu Bongo ambaye alitumia vyema kujulikana kwake kisanii kwenda Kigoma kuomba Udiwani wa Kata ya Mwanga kupitia ACT- Wazalendo ambako alishinda kirahisi.

 

14 : MIKE

Watu wengi ukitaja jina la Mike Sangu watajua ni msanii aliyekuwa mume wa mwigizaji Thea, ni kweli ndiko alikochomozea nyota yake lakini kwa sasa anafanya kazi ya siasa kupitia CCM. Anatajwa kuwa ni Katibu Mwenezi wa Kata ya Mburahati, Dar na dereva wa Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye.

15 : CHIKOKA

Juma Chikoka alianza kuwika kwenye maigizo l akini baadaye alijitosa pia kwenye siasa ndani ya chama tawala ambako kwa sasa ni miongoni mwa viongozi wa hamasa ndani ya umoja wa vijana wa chama hicho.

Comments are closed.