LE MUTUZ AOMBEWA AFYA

KUTETELEKA kwa afya ya Mwanablogu maarufu nchini, William Malecela a.k.a Le-Mutuz kulikosababisha alazwe Hospitali ya Taifa Muhimbili; Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, kumeibua maombi kila kona ya kumtakia apone haraka.

 

Risasi Mchanganyiko limebaini kuwa, kanda mbalimbali za watu kupitia njia ya mitandao ya kijamii pamoja na kufika hospitalini alikolazwa wamekuwa wakishiriki kumuombea Le- Mutuz ili aweze kupona jambo ambalo mwenyewe amekuwa akilishukuru.

Kwenye mitandao ya kijamii, ”Get Well Soon”, “Mungu akuponye mpiganaji” ni miongoni mwa maneno yaliyotumika na wadau wengi walipoposti komenti zao kwenye mtandao wake wa Instagram anaotumia kuwahabarisha watu kuhusu maendeleo ya afya yake. “Pole big mwenzangu Mungu ndiyo kila kitu, inshaallah utapona,” aliandika posti yake mtu alijitambulisha kwa jina la ramsomsaki.

Kutokana na maombi hayo Le-Mutuz amekuwa akiwashukuru wote wanaomuombea afya njema na kuongeza kuwa anafarijika kuona watu wengi wako nyuma yake. “Nashukuru kwa maombi, naendelea vizuri, Nimonia ilikuwa imenikamata, si unajua haya Ma- AC yanasababisha tatizo kwenye mapafu,” alisema Le- Mutuz alipozungumza na Risasi Mchanganyiko jana (Jumanne) kwa njia ya simu.

Tangu alazwe, watu mbalimbali wakiwemo wanasiasa na mastaa wamefika hospitalini hapo kumjulia hali akiwemo baba yake mzazi na Mwanablog huyo, mzee John Samuel Malecela. Wengine ni msanii Steve Nyerere, Blandina Chagula ‘Johari’, Nasib Abdul ‘Diamond’, Jacob Steven ‘JB’ na Mrisho Mpoto.


Loading...

Toa comment