The House of Favourite Newspapers

Lema Ataka Naibu Spika Ashughulikiwe kwa Kuimba ‘Nyegezi Mwanza’ – VIDEO

Video inayosambaa mtandaoni ikimuonyesha Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson akiwa na wabunge wanzake wakiimba wimbo ‘Mwanza’ wa mwanamuziki Rayvanny akimshirikisha Diamond Platnumz ambao umefungiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), imezua gumzo mtandaoni.
Wabunge hao walikuwa nchini Burundi kwenye michuano ya wabunge na baada ya kuibuka na ushindi wakaanza kushangilia kwa style ya kuimba wimbo huo ambao upo kifungoni.
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amefunguka kwa kudai kwamba, Spika Tulia anatakiwa kuhojiwa na kamati ya maadili ya Bunge kuhusiana na tukio hilo.
“Nina muomba Mh Spika Ndugai aitishe kamati ya maadili ya Bunge juu ya kitendo cha Naibu Spika Mh Tulia kuimba na kucheza wimbo uliopigwa marufuku na Basata unaoitwa Nyege,Nyege ,Nyegezi /Mwanza akiwa Nchini Burundi.Mimi na Mke wangu tume huzunika sana”.
Kupitia Ukurasa wake wa Instagram, Diamond ameweka video hiyo na kuandika;

Comments are closed.