The House of Favourite Newspapers

Ligi ya Wanawake… Moto Unawaka si Mchezo

LIGI Kuu ya Wanawake Tanzania Bara inaendelea kushika kasi huku ushindani mkali ukijitokeza mapema tu. Timu shiriki kwenye ligi hiyo maarufu kama Serengeti Lite Women’s Premier League 2018/19, ni 12.

Bingwa mtetezi wa ligi hiyo ni JKT Queens iliyoutwaa ubingwa huo msimu uliopita na kuziacha timu zingine kama Simba kushindwa la kufanya.

Katika msimu huu ulioanza Desemba 29, mwaka jana, mpaka sasa zimechezwa mechi tatu kwa kila timu.
Ikiwa ni mapema tu, kuna mambo makubwa yamefanyika ikiwemo mechi moja kumalizika kwa ushindi mnono wa mabao 16-0. Ni ushindi mkubwa katika ligi hiyo.


Ushindi huo ulipatikana kwenye Uwanja wa Jenerali Isamuyo uliopo Dar ambapo wenyeji, JKT Queens waliifunga Mapinduzi Queens, Jumapili iliyopita.
Leo Championi Jumatano linakuchambulia mechi za ligi hiyo na hali ilivyo tangu kuanza kwa msimu huu.

 

Vinara wa ligi
Hadi kufikia juzi Jumatatu, mabingwa watetezi wa ligi hiyo, JKT Queens walikuwa wanaongoza kufuatia kushinda mechi zote tatu walizocheza hadi sasa. JKT katika mechi yao ya kwanza dhidi ya Evergreen, walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 9-0, kisha wakaichapa Tanzanite SC mabao 6-0, mechi ya tatu wakaitungua Mapinduzi Queens mabao 16-0.

Mpaka sasa, timu hiyo imefanikiwa kufunga jumla ya mabao 31 huku yenyewe ikiwa haijafungwa bao lolote na imejikusanyia pointi tisa.

Wakati JKT wakiongoza, Mlandizi Queens wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi saba baada ya kushinda mechi mbili na kutoka sare moja. Wana pointi sawa na Simba Queens lakini tofauti yao ni mabao ya kufunga na kufungwa. Simba inashika nafasi ya tatu.

Timu iliyofungwa mabao mengi
Katika ligi hiyo, Mapinduzi Queens mpaka sasa ndiyo wanaonekana kuwa vibonde kutokana na kufungwa mabao 29 katika mechi zake tatu.
Timu hiyo ndiyo inaburuza mkia baada kukubali kichapo cha mabao 6-0 kutoka kwa Mlandizi Queens, kisha ikafungwa mabao 7-0 na Panama, ikaja kufungwa na JKT Queens mabao 16-0.

Kinara wa mabao
Mshambuliaji wa JKT Queens, Fatuma Mustapha ndiye kinara wa mabao katika ligi hiyo akiwa amefunga mabao 15 katika mechi tatu alizocheza na kikosi chake cha JKT.
Fatuma anafuatiwa na mshambuliaji matata wa siku nyingi akitokea kwenye timu hiyo, Asha Rashid ‘Mwalala’ mwenye mabao saba.

 

HAT TRICK KAMA ZOTE
Mbali ya wafungaji hao kitu pekee kinachovutia katika ligi hiyo kitendo cha washambuliaji kuwa na njaa ya kufunga mabao mengi katika mchezo mchezo mmoja.

Kinara wa ufungaji mabao kutoka JKT Queens, Fatuma Mustapha ameshafunga hat trick tatu katika mechi zote tatu alicheza.
Akifuatiwa na Asha Rashid ‘Mwalala’ na Donisia Minja ambao wote wanatokea JKT kwa kila mmoja akiwa amefunga hat trick moja katika mechi tatu huku safu yao ya ushambuliaji ikionekana kuwa ni kiwembe kutokana na kufunga mabao mengi kwenye ligi hiyo kuliko timu yoyote mpaka sasa tangu kuanza kwa ligi hiyo msimu huu.

 

WANAPUMULIA GESI
Tanzanite, Baobab Queens na Mapinduzi timu pekee ambazo zimepoteza mechi tatu za kwanza katika ligi hiyo wakiwa kwenye nafasi tatu za chini katika msimamo wa ligi hiyo bila ya kuwa na pointi yoyote.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

KARIBU ujiunge na familia ya marafiki wa Global TV Online – Club sasa, uwe wa kwanza kupata video zote za Global TV, video za hamasa kutoka kwa Eric Shigongo, breaking news za matukio yote duniani, michezo na dondoo za afya. Utapata nafasi ya kuingia bure na kutazama shoo, matamasha, semina na burudani zinazoandaliwa na Global TV mikoa yote Tanzania.
Pia, ukiwa na tatizo la kifamilia mfano misiba, kuuguliwa na majanga, marafiki zako wa Global TV Club tutakusaidia.
 
Pia, tutakuunganisha na mtandao wa marafiki zetu waliyofanikiwa ndani na nje ya Tanzania, ili upate mafunzo maalum ya kujikwamua kutoka katika hali duni ya maisha.

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.