JPM Aanika Alivyosoma Meseji za Waziri Akitifuana na Katibu Mkuu – Video

RAIS John Magufuli amewataka viongozi na watumishi wote wa serikali kuacha malumbano na badala yake kushirikiana katika kutekeleza miradi mbalimbali ili kuleta maendeleo kwa wananchi wote.

 

Magufuli amesema hayo leo Jumatano, Januari 9, 2019 baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua jana.

 

“Nilikuwa nafuatilia meseji za Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na Katibu Mkuu wa TAMISEMI (Dkt. Zainabu Chaula) anayeshughulikia afya, nikaona wanavyorushiana maneno wee, mwigine ananyamaza lakini mwenzake anamshindilia maneno tu, nikasema hawa njia ya kuwakomesha ni kuwaweka wizara moja, akakae na dada yake.  Wote wanatoka Tanga.

 

Rais Magufuli akimuapisha Dkt. Zainabu Chaula kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (anayeshughulikia afya). Kabla ya Uapishohuo Dkt. Chaula alikuwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI (afya).

 

Akitoa mfano mwingine wa viongozi kutoelewana alisema:

“Nafahamu zipo halmashauri ambazo viongozi wanagombana mfano; Nyasa wanagombana sana DC na Mkurugenzi nimewaangalia tu! Nimewaachia kiporo chao.  Kuna Gairo, DC na mbunge,  mpaka mbunge ana-post ujumbe wa kumtukana DC tena mke wa mtu, hajui kama anaweza kupoteza ubunge… I hope siku moja ataomba msamaha kwenye Bunge.”

 

Mifano mingine aliyotoa ni ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma na Mkuu wa Wilaya ambao amewaonya na akasema “wamenyamaza naona yameisha.”

 

Magufuli akimuapisha Dkt. Dorothy Gwajima kuwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI (Afya). Kabla ya Uapisho huo Dkt. Gwajima alikuwa Mkurugenzi wa Tiba wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

 

Pia Magufuli aliwachekesha wasikilizaji wake pale aliposema kwamba pamoja na mapungufu makubwa katika balozi za Tanzania, aliamua kumchukua aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya awe balozi kwa vile ameonyesha kusafiri sana kwenda nchi za nje.

 

“Tuna mapungufu makubwa katika balozi zetu, hivyo, ili kuimarisha hali hiyo nikaona nimchukue Katibu Mkuu wa Afya kwa sababu yeye ndiyo amesafiri sana kwenda nje. Nikaona bora akakae hukohuko nje.   Wizara ya Afya ina mikutano mingi ya nje lakini jamaa hakutaka hata ku-delegate (kuwaachia wengine fursa ya kusafiri nje),” alisema Magufuli.

 

Aidha, aliwataka watendaji wasizichukulie wizara kama mali zao na wafanye maamuzi kwa maslahi ya nchi na kwa mujibu wa sheria.

TAZAMA VIDEO HII

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

KARIBU ujiunge na familia ya marafiki wa Global TV Online – Club sasa, uwe wa kwanza kupata video zote za Global TV, video za hamasa kutoka kwa Eric Shigongo, breaking news za matukio yote duniani, michezo na dondoo za afya. Utapata nafasi ya kuingia bure na kutazama shoo, matamasha, semina na burudani zinazoandaliwa na Global TV mikoa yote Tanzania.
Pia, ukiwa na tatizo la kifamilia mfano misiba, kuuguliwa na majanga, marafiki zako wa Global TV Club tutakusaidia.
 
Pia, tutakuunganisha na mtandao wa marafiki zetu waliyofanikiwa ndani na nje ya Tanzania, ili upate mafunzo maalum ya kujikwamua kutoka katika hali duni ya maisha.

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Loading...

Toa comment