The House of Favourite Newspapers

Akili ya Linnah ya Utoto, Hiki Ndo Alichomuiga Mama Yake!

MWANAMUZIKI Estelina Sanga ‘Linah’ kwa mara ya kwanza amefunguka siri ambayo hajawahi kuisema kuwa enzi za utoto wake alikuwa anapenda sana kuokota nyuzi na kushonashona vitambaa vya kutandika ndani, hali iliyomfanya ashindwe kufanya vitu vingine vya maana.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, msanii huyo alisema tabia hiyo ilitokana na hulka ya mama yake ambaye mara nyingi ilikuwa akitoka kazini anakaa na kuanza kufuma vitambaa ambavyo ndio alikuwa akivitandika sebuleni kwao.

“Katika udogo wangu mara nyingi nilikuwa nikimuiga mama kushonashona, hata kazi nyingine nilikuwa sifanyi utanikuta najishonea tu, nadhani wengi wanajua mambo ya kushona na akili inakuwa haiwazi mambo mengine ya maana,” alisema Linah ambaye anadai yeye hakucheza sana ile michezo ya kitotototo.

STORI: MEMORISE RICHARD

Comments are closed.