The House of Favourite Newspapers

Yanga na Chirwa watauana

TANGU mwaka jana Azam na Yanga wamekutana mara tatu kwenye mashindano mbalimbali lakini takwimu zinaibeba Azam.

 

Timu hizo zinapamba kesho Jumatatu kwenye mechi ya Ligi itakayopigwa ndani ya Uwanja wa Uhuru badala ya Taifa ambao unapumzishwa baada ya kutumika muda mrefu. Katika mechi ya awali mwaka jana, Yanga
ilishinda mabao 2-1

Januari lakini zilipokutana Mei, Yanga akala 3-1. Mapema mwaka huu zikakutana kwenye Mapinduzi Yanga ikiwa na kikosi cha vijana ikachapwa mabao 3-0. Msimu huu timu hizo hazijacheza mechi hata moja kutokana na ratiba
kupanguliwa mara kwa mara.

 

Yanga wanaingia kwenye mchezo wa kesho wakiwa na kikosi cha chote baada ya wachezaji kusitisha mgomo baridi waliouitisha wakishinikiza kuonana na viongozi kudai chao.

Mtihani mkubwa utakuwa kwa makocha wawili Mwinyi Zahera wa Yanga na Idd Cheche wa Azam ambae amekuwa kwenye fomu nzuri tangu akabidhiwe kuiongoza timu hiyo kwa muda.

 

Ushindi kwenye mchezo huo ni muhimu kwa timu yoyote kutokana na mchuano mkali ulioko katika nafasi tatu za juu kwenye msimamo wa Ligi inayoongozwa na Yanga wenye pointi 74.

 

Mafowadi wa Azam ambao ni Wachezaji waliomwagwa na Yanga,Donald Ngoma na Obrey Chirwa wamepania kushinda mchezo huo ili kukata ngebe za Yanga ambao walipuuza kile kipigo cha Mapinduzi kwa madai kuwa ilikuwa timu ya vijana.

 

Lakini Yanga, Heritier Makambo na Amissi Tambwe wamepania kumziba mdomo,Cheche ambae anajiita Ole Gunna. Ligi Kuu ya Bara kama haitapanguliwa tena, itafikia tamati Mei 28.

Comments are closed.