The House of Favourite Newspapers

LINEX AFUNGUKA KUPORWA MTOTO WAKE

Sunday Sangu ‘Linex’

MKALI wa Bongo Fleva, Sunday Sangu ‘Linex’ amefungukia kinachomuumiza kwa sasa ni kitendo cha kunyang’anywa mtoto na mzazi mwenziye.

Akizungumza na Mikito Nusu Nusu, Linex alisema kuwa hajamuona mtoto wake huyo wa kiume takribani miaka minne iliyopita tangu aliponyang’anywa nyumbani kwa mama yake.

“Yaani kinachoniuma mtoto wangu ana miaka 12 sasa, najua angekuwa na furaha sana ya kuwa na mimi lakini mpaka sasa sijui alipo wala pakumpata maana mama yake mpaka simu kabadilisha nasikia tu anaishi Kahama, nina hamu sana na mwanangu,” alisema Linex

Stori: Imelda Mtema

Comments are closed.