The House of Favourite Newspapers

Linex amfungukia video queen wake!

0

erycahErycah

IMELDA MTEMA

STAA wa Bongo Fleva anayetikisa na Ngoma ya Hewala, Sunday Mangu ‘Linex’ kwa mara ya kwanza amemfungukia aliyekuwa mpenzi na video queen wake, Ericka Daniel ‘Erycah’ kuwa amlaumu kwa kumuacha.

LinexSunday Mangu ‘Linex’

Akizungumza na Showbiz Extra Linex alisema kuwa, anajua fika kipindi alichokuwa na Erycah wanaume wengi walikuwa wanamsumbua kwa sababu tu wamemuona yuko kwenye uhusiano na staa.

“Unajua watu ni wa ajabu sana wanaweza wakampenda mwanamke kwa sababu tu yuko na staa bila kujua yule aliyenaye naye alikuwa na vigezo vya kuwa na mwanamke huyo. Sina maana namlaumu Erycah kuniacha na kuendelea na maisha mengine ya kimapenzi, hapana! Binadamu wengi lazima tupitie hali hiyo,” alisema Linex.

Erycah alianza kuonekana kwa mara ya kwanza katika Video ya Kwa Hela ya Linex kisha kudaiwa kuwa wapenzi.

Leave A Reply