The House of Favourite Newspapers

Lionel Messi Akubali Kuongeza Mkataba PSG Baada ya Ubingwa wa Kombe la Dunia

0

 

Lionel Messi.

NAHODHA wa Argentina, Lionel Messi amefikia makubaliano binafasi ya kuongeza mkataba wa kuendelea kubakia Paris St-Germain, kwa mujibu wa taarifa ya Guillem Balague wa BBC Sport.

Messi, 35, ambaye aliiongoza Argentina kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia nchini Qatar, mkataba wake na PSG unamalizika Juni 2023.

Mapema wiki hii Rais wa Barcelona, Joan Laporta alisema angependa Messi arejee katika klabu hiyo ya Hispania ambako alikaa kwa miaka 21.

Lakini Balague anasema Barca hawajawasiliana na Messi kuhusu kurejea.

Messi atasaini mkataba wa mwaka mmoja na chaguo la mwaka mwingine na makubaliano hayo yamekuja baada ya miezi minne ya mazungumzo kati ya mkurugenzi wa soka wa PSG, Luis Campos na baba yake Messi, Jorge.

Mwenyekiti wa PSG, Nasser Al-Khelaifi alifanya kikao kizito na Messi kule Doha Qatar wakati wa Kombe la Dunia na wakafikia makubaliano hayo.

“Kwa kweli yote yamekubaliwa na PSG,” anasema mtaalam wa soka wa Ulaya Balague na kuongeza: “Barcelona haijamkaribia yeye au baba yake na kusema chochote.

“Kwa hiyo si kwamba Messi hataki kurejea Barcelona. Hajapata ofa hiyo.”

#EXCLUSIVE: MREMBO ALIYENYANYUA KIBAO cha ROUND KWENYE PAMBANO la MANDONGA na ALIBABA…

Leave A Reply