The House of Favourite Newspapers

Lionel Messi Atupwa Nje kwa Mara ya Kwanza katika Kinyang’anyiro cha Ballon d’Or

0
Lionel Messi

HUENDA ikawa habari mbaya kwa staa wa PSG Muargentina Lionel Messi baada ya kukosekana kwenye orodha ya wachezaji 30 wanaowania tuzo ya Balon d’Or hii ikiwa ni kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2005.

Hasimu wa karibu wa Messi mshambuliaji wa Manchester United Cristiano Ronaldo akiwa amejumuishwa kwenye orodha hiyo pamoja na Mohamed Salah, Erling Haaland na Karim Benzema.

Messi anaongoza kwa kushinda tuzo hiyo akifanikiwa kuinyakua mara saba huku Ronaldo akichukua mara tano.

Cristiano Ronaldo

Jumla ya wachezaji walio orodheshwa katika idadi ya wachezaji bora 30 wanaowania tuzo ya Ballon d’Or ni Cristiano Ronaldo, Harry Kane, Trent Alexander Arnold, Phil Foden, Kevin De Bruyne, Erling Haaland, Mohamed Salah, Luiz Diaz, Fabinho, Virgil Van Dijk, Darwin Nunez, Sadio Mane, Heung Min Son, Thibaut Coutouis, Karim Benzema, Rafael leao, Christopher Nkunku, Joshua Kimmich, Vinicius Jr, Bernardo Silva, Robert Lewandowski, Riyad Mahrez, Casemiro, Mike Maignan, Sebastien Haller, Luka Modric, Antonio Rudiger, Dusan Vlahovic, Joao Cancelo pamoja na Kylian Mbappe.

Leave A Reply