The House of Favourite Newspapers

Lissu Atakiwa Kuripoti Ofisi Ya Mkurugenzi Wa Mashtaka Kufuatia Kauli Zake – Video

0
Tundu Lissu

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amedai kuitwa na Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum Dar es Salaam kesho tarehe 20 Julai 2023.

Kwa mujibu wa barua iliyotolewa jana tarehe 18 Julai 2023 kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), ilimtaka Mwanasheria huyo machachari kufika katika ofisi hiyo kutokana na kauli alizozitoa tarehe 15 Julai 2023 na kusambazwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Tarehe 15 Julai 2023, Lissu anadaiwa kutumia maneno yasiyo na staha kumjibu Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu uwekezaji wa Kampuni ya DP World katika bandari ya Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa barua hiyo ya wito, Lissu anatakiwa kufika kwa mahojiano ili kukamilisha uchunguzi wa maneno hayo.

Kupitia ukurasa rasmi wa akaunti yake ya Twitter, Lissu ameandika hivi; “Baada ya mawakili Mwabukusi, Madeleka & Ruge Nshala, sasa ni zamu yangu. DCI Kingai ametuma watu kuleta barua ya kuripoti ofisini kwake. Wamerudi nayo baada ya kujulishwa niko nje ya nchi. Nitarudi wiki ijayo kuwakabili. Madalali wa bandari zetu wasitutishe”.

Leave A Reply