The House of Favourite Newspapers

Litakavyofanyika Tamasha la Pasaka Mwaka Huu, Msama Afunguka! – VIDEO

Mkurugenzi wa Tamasha la pasaka nchini, Alex Msama ameeleza namna watakavyotumia tamasha la pasaka mwaka 2019 kueleza kwa wananchi mambo ya maendeleo ambayo yamefanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli.

Akiongea katika mkutano wake na waandishi wa habari, Msama amesema mambo ambayo serikali ya awamu ya tano imefanya ni mengi na yanapaswa kufahamika na wanachi ili kujua kinachoendelea katika nchi yao.

Aidha katika hatua nyinge, Msama amewataka wasanii wote nchini kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia maadili na miongozo ya baraza la sana nchini Tamasha la pasaka linatarajiwa kufanyika mwezi April likianzia jijini Dar es Salaam na kufuatiwa na ziara ya nchi nzima

Comments are closed.