The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Aweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Daraja la Rau – Video

0

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi katika Daraja la Rau, linalounganisha Moshi vijijini na Moshi mjini, linalotarajiwa kugharimu Sh900 milioni hadi kukamilika.

 

Daraja hilo ambalo lilisombwa na mafuriko mwaka juzi, linatarajiwa kukamilika Januari 2022 na kurudisha matumaini kwa wananchi waliopata adha kubwa kutokana na ukosefu wa daraja.

 

Kukosekana kwa daraja hilo, kulisababisha adha kubwa kwa wananchi wanaotoka maeneo ya Uru,Moshi vijijini kwenda kufanya shughuli za uzalishaji mali Moshi mjini, huku wagonjwa wakilazimika kutumia gharama kubwa kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za afya.

 

Akizungumza baada ya kuweka jiwe hilo la msingi, Rais Samia amesema anatambua shida walizokuwa wakipata wananchi wa maeneo hayo kutokana na kukosekana kwa daraja hilo. Amesema daraja limefikia hatua nzuri na Serikali itamalizia fedha zilizobaki ili kukamilisha ujenzi huo kwa wakati uliokusudiwa.

 

Rais Samia amewaondoa hofu wananchi na kuwataka kuendelea kuiamini Serikali na kwamba atahakikisha changamoto zote zinazowakabili zinapatiwa ufumbuzi.

 

“Natambua zipo changamoto za miundombinu ya barabara, ikiwamo Barabara ya Rau -Mamboleo-Materuni Kilomita 10, Mamboleo-Rehan-Shimbwe Kilomita 13.4 na Barabara ya Rehan_mruhia, niwaahidi ifikapo mwaka 2025, tutakuwa tumetengeneza barabara hizi, “amesema Rais Samia. 

 

Leave A Reply