The House of Favourite Newspapers

Yanga yashinda bao 2-1dhidi ya APR

1
 CdW7L50UEAEVOyT.jpg large
MPIRA UMEKWISHAAA
-GOOOOOO Dakika za majeruhi, Patrick Sibomana anaifungia APR bao moja
-Mugenzi anapoteza nafasi ya wazi kabisa baada ya krosi safi kutoka Magharibi ya uwanja
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 89, nusura Msuva afunge bao la tatu baada ya kipa na mabeki wa APR kujichanganya
SUB Dk 87 Yanga inamtoa Niyonzima na kumuingiza Mbuyu Twite
KADI Dk 85, Juma Abdul analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Bizimana
Dk 83 Emiry anapiga mpira wa adhabu unavuka ukuta wa Yanga lakini Barthez anadaka vizuri kabisa
Dk 81, APR wanapata kona ya saba katika kipindi cha pili pekee, anaichonga Iranzi, lakini inakuwa haina manufaa kwa mara nyingi. APR sasa wanaonekana kutoka mchezoni zaidi wanafanya ubabe tu
CdW0AQ7W4AA8IKT.jpg large
Dk 81, APR wanapata kona ya saba katika kipindi cha pili pekee, anaichonga Iranzi, lakini inakuwa haina manufaa kwa mara nyingi. APR sasa wanaonekana kutoka mchezoni zaidi wanafanya ubabe tu

DK 80, Free kick, Juma Abdul anapiga vizuri kabisa, hata hivyo anashindwa kulenga lango
KADI Dk 78 Emiry Bayisenge analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Ngoma
Dk 77 APR wanapata kona nyingine baada ya Yanga kuokoa, lakini inaonekana haina matunda
GOOOOOO Dk 74, Kamusoko anaifungia Yanga bao la pili baada ya Juma Abdul kumpa pasi Ngoma aliyempasia mfungaji kwa ulaini kabisa
Dk 71 sasa bado inaonekana mpira zaidi unakuwa wa kubutua, unachezwa zaidi katikati ya uwanja na Ngoma leo anaonekana kutokuwa na mchango mkubwa na amepooza sana
Dk 67 sasa, kinachoonekana Yanga wamepoozesha mchezo lakini APR wanashambulia zaidi na sasa wamepata kona tano katika kipindi cha pili pekeeDk 66, kona safi ya APR inachongwa na Bernabe anapoteza nafasi nyingi ya wazi wakati Barthez akiwa amelala chini baada ya kugongwa
Dk 64, Yanga wanapata kona ya kwanza katika kipindi cha pili, hata hivyo inakuwa ni dhaifu na isiyo na matunda
Dk 60, Yanga wanafanya shambulizi kali la kipindi cha pili, lakini APR wanaokoa na mpira unagonga mikono ya MsuvaKADI Dk 57 Iranzi analambwa kadi ya njano kwa kumsukuma Yondani kwa makusudi
Dk 55 APR wanapata kona ya pili, shuti kali linapigwa lakini mpira unaokolewa na pato Ngoyani anayepiga kichwa shuti hilo linalomwangusha, yuko chini anatibiwaDk 51 APR wanatumia muda mwingi kucheza mpira katika eneo lao. Bado inaonekana hata Yanga pia hakuna mashambulizi makubwa wanayofanya na kusababisha mpira kuonekana umepoa sana
Dk 48, Iranzi kabisa lakini Yondani anaokoa na kuwa kona lakini haina matundaDk 47 krosi nzuri Rutanga anaiwahi na kuugonga mpira lakini Barthez anauwahi na kudaka vizuri
SUB Dk 46 Yanga inamtoa Tambwe ambaye mwanzo ilielezwa ni majeruhi na nafasi yake inachukuliwa na Simon MsuvaMAPUMZIKO
Dk 45, Juma Abdul anafanya uzembe mkubwa, Mwinyi anaokoa na kuwa kona. APR wanapiga lakini Barthez anaruka safi kabisa na kudaka vizuuuriiiDk 42 Bizimana ambaye ni mjomba wa Niyonzima anapoteza nafasi nzuri kabisa ya kufunga baada ya kuruka na kushindwa kupiga kichwa akiwa pekee analiangalia lango la Yanga
Dk 37, Juma Abdul anaruka kupiga kichwa krosi safi ya Mwinyi, hata hivyo anashindwa kuufikia mpira, anafanya madhambiDk 34, shuti kali la kwanza kumfikia kipa linapigwa na Iranzi, lakini Barthez anaonyesha umahiri kwa kudaka vizuri kabisa
Dk 32, Juma Abdul analala chini baada ya kuumia, Pato Ngonyani ndiye aliyemkanyaga kwa bahati mbaya wakati wakiwania mpira
Dk 29, Iranzi anaonekana kulalamika, kwamba hakumuangusha Niyonzima ambaye alikuwa akiwachambua. Niyonzima anaonekana kupania kuonyesha mambo mengi katika mechi hii ambayo amerejea nyumbani akiwa na Yanga
Dk 22, Bernabe maarufu kama Balotelli anaruka juu na kupiga kichwa safi kabisa, lakini kinakuwa hakina nguvu na Barthez anadaka kwa ulaini kabisa
GOOOOOOOOO Dk 20 Juma Abdul Jaffar anaiandikia Yanga bao la kwanza kwa mpira safi wa faulo

Dk 18, Juma Abdul anakunja krosi safi kabisa, lakini hata hivyo inakuwa juu kidogo, Tambwe anashindwa kuiwahi
Dk 12 hadi 14, bado inaonekana ni mechi ya kuviziana, kidogo beki wa kushoto wa Yanga, Mwinyi Haji anaonekana kutotulia vizuri na ndani ya dakika mbili amepoteza mipira mitatu

Dk 11, kona ya kwanza ya mchezo, APR ndiyo wanaopata lakini inaokolewa vizuri hapa na Yondani
Dk ya 10 sasa, bado hakuna timu iliyoonyesha kuwa na mpango madhubuti katika ushambulizi. Huenda ni hofu ya mwanzo ya mchezo huku APR wakionekana kupoteza sana mipira
Dk 9, Bernabe wa APR naye katika nafasi nzuri pembeni ya uwanja anapiga shuti la hoovyoo kabisa
Dk 4, Kaseke anajaribu kupiga shuti lakini linakuwa dhaifu kabisa

Dk 1, APR ndiyo wanaanza pambano kwa kasi, lakini Yanga wanaonekana kuupoza mpira

KIKOSI CHA APR

1. Kwizera Oliver
2. Rusheshangoga
3. Michael  Rutanga
4. Eric Rwatubyaye
5. Emiry Bayisenge
6. Yannick Mukunzi
7. Fisto Kinzingabo
8. Jihadi Bizimana (Mpwa wa Haruna)
9. Mubumbyi Bernabe
10. Iranzi Jean Claude (C)
11. Patrick Sibomana.
#Subs
1.Ndoli Jean Claude
2.Rwigema Yves
3.Usengimana Faustin
4.Nshutinamagara Ismael
5.Benedata Jamvier
6.Mugenzi Biemveni

 

7.Ntamuhanga Tumaini
KIKOSI CHA YANGA:
1. Ally mustapha
2. Juma abdul
3. Mwinyi haji
4. Calvin yondani
5. Vincent bossou (C)
6. Pato ngonyani
7. Deus kaseke
8. Thaban kamusoko
9. Hamis tambwe
10. Donald ngoma
11. Haruna niyonzima
Formation 3:5:2
Subs
1. Deo munis
2. Oscar joshua
3. Mbuyu twitte
4. Issouf boubakr
5. Salum telela
6. Matheo anthony
7. Simon msuva
1 Comment
  1. Solomon Nyandind says

    Daaah! kwa mwendo huo Jangwan mmenifurahisha ile kinoma noma

Leave A Reply