The House of Favourite Newspapers

Pichaz + Video: Gor Mahia Wababe SportPesa Super Cup, Wamewafunga AFC Leopards Mabao 3-0

0

 

KIKOSI cha Gor Mahia cha Kenya leo Jumapili kimefanikiwa kuibuka mabingwa wa michuano ya SportPesa Super Cup baada ya kuwafunga ndugu zao, AFC Leopards kwenye ‘derby ya Mashemeji’ iliyopigwa Uwanja wa Uhuru, Dar.
Gor Mahia wamewafunga AFC Leopards kwa mabao 3-0 na kufanikiwa kuwa mabingwa wa kombe hilo kwa mara ya kwanza ambapo wamefanikiwa kuchukua kombe pamoja na fedha zaidi ya milioni 60.

Pia kikosi hicho kitapata nafasi ya kucheza na timu ya Everton inayoshiriki Ligi Kuu ya England baadae mwezi ujao. Safari ya mabingwa hao ilianza kwa kuwatoa Jang’ombe Boys ya Zanzibar kwa mabao 2-0 kisha wakawafunga Nakuru All Stars kwa mabao 2-0 na kumaliza na Leopards.

(PICHA: RICHARD BUKOS/GPL)

Leave A Reply