The House of Favourite Newspapers

Full Time: Gwambina Fc Vs Simba Sc ( 0 – 1 ) – Ligi Kuu Bara

0

KOCHA Msaidizi wa Simba, Seleman Matola amesema kikosi chake kinaenda kukutana na mchezo mgumu dhidi ya Gwambina bila wachezaji wake watatu muhimu wa kikosi cha kwanza.

Simba leo watakuwa wageni wa Gwambina kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na Waandishi wa Habari kuelekea kwenye mchezo wa leo, Matola aliwataja wachezaji watakaokosekana leo kuwa ni Thadeo Lwanga, Luís Miquissone, na Paschal Wawa ambao wanatumikia kadi tatu za njano kwa kila mmoja .

 

Matola pia alieleza gazeti hili kuwa, licha ya kukosekana kwa wachezaji hao muhimu bado wamejiandaa vya kutosha kuhakikisha wanabeba alama tatu.“Tunatumbua kuwa Gwambina ina uwanja mbovu ambao hauchezeki lakini tumejiandaa kwa hilo na tunaamini kuwa tutatumia mbinu mbadala kuhakikisha tunapata matokeo ili tuweze kuongoza ligi,” alisema Matola

Leave A Reply